Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Bw. Godfrey Chibulunje akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam.
************************
Na Noel Rukanuga – Dar es salaam.
Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA) imevifungia vituo ya mafuta 26 na kuvitoza faini kwa kosa la kukwepa kodi pamoja na kukutwa na mafuta yasiyo vinasaba.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es salaam, Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa EWURA Bw. Godfrey Chibulunje, amesema kuwa zoezi la ukaguzi lilianza julai 2 mwaka huu na lilifanyika katika mikoa ya kanda ya mashariki (Dar es salaam na Pwani, kanda ya Ziwa ,kanda za juu kusini, kanda ya kati ambapo hadi kufikia agosti 9 mwaka huu .
Bw. Chibulunje amesema kuwa jumla ya vituo 195 vya matufa walifanikiwa kukagua ambapo vituo 26 sawa asilimia 13.33 vilikutwa na mafuta ambayo hayana kiwango stahiki cha vinasaba.
Amevitaja baadhi ya vituo hivyo ni pamoja na Lake oil Company cha Geita, GBP Oill Mwanza, Total Tanzani Mwanza, Azhad Abdulrahim Mkuranga, Ally Adon ya Mombasa.
“Kwa mujibu wa kanuni kampuni zenye depots zinatakiwa kuhakikisha mafuta yote yaliyonunuliwa kwa ajili ya soko la ndani yanawekewa vinasaba na Mfanyabiashara yeyote anayenunua mafuta anatakiwa kuhakikisha yanawekwa vinasaba kwa usahihi kwenye gari likilobeba mafuta” amesema Chibulunje.
Amesema kuwa baada ya Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kukabidhi EWURA mashine za kung’amua vinasaba kwenye mafuta (Fuel marker dectection machine) ilianza zoezi la ukaguzi kwenye vituo vya mafuta ili kuhakiki kama mafuta kwenye vituo hivyo yana kiwango sahihi cha vya vinasaba.
Mkurugenzi amewaasa wafanyabiashara wote kufanyabiashara zao kwa kufuata taratibu za sheria zilizowekwa ili kuepuka usumbufu usiokuwa wa lazima.