Meneja wa Wilaya ya Chato Bw.Nyaonge Nyabinyiri akitoa maelezo kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Geoffrey Mwambe mara baada ya kutembelea banda la TANESCO wakati wa maonesho ya Utalii na Biashara yanayofanyika Chato.
Baadhi ya wafanyakazi wa TANESCO wakiwa katika banda lao wakati wa maonesho ya Utalii na Biashara yanayofanyika Chato.
Muonekano wa Banda la TANESCO katika Maonesho ya Utalii na Biashara yanayofanyika Chato.
…………………………………………………………
Shirika la Umeme nchini (TANESCO) limeshiriki katika maonesho ya Utalii na Biashara Chato ikiwa ni mdau muhimu kwenye kuvutia uwekezaji Chato.
Maonesho hayo yameanza Agosti 7, mwaka na kufunguliwa leo Agosti, 11,2021 na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uwekezaji Geoffrey Mwambe.
Shirika hilo limewahakikishia wananchi na wafanyabiashara uhakika wa umeme wa kutosha ili kuwekeza wilayani Chato Mkoani Geita.
Katika banda la TANESCO wananchi wanaweza kujionea kifaa cha UMETA ,ambacho wataalamu wanaonyesha hatua zote kuanzia maombi ya umeme hadi hatua ya mwisho umeme unapomfikia mteja.
Pia wananchi wamelisifu Shirika hilo kwa hali ya upatikanaji umeme kwa hivi sasa.
“Kwa kweli mnastahili pongezi, tulikuwa katika shida kubwa ya kupata umeme wa uhakika kwa muda mrefu, lakini hali kwa sasa imebadilika sana, umeme hausumbui kama ilivyokuwa hapo awali.” wamesema wananchi
Kilele cha maonesho hayo kitakuwa Agosti, 15 mwaka huu