Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt Philemon Sengati akiongea na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kupitia Radio Gold FM muda mchache baada ya kushiriki uzinduzi wa kipindi kipya Gold Breakfast cha radio hiyo kilichoanza kwenda hewani kuanzio leo katika Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt Philemon Sengati akiongea na wananchi wa Mkoa wa Shinyanga kupitia Radio Gold FM muda mchache baada ya kushiriki uzinduzi wa kipindi kipya Gold Breakfast cha radio hiyo kilichoanza kwenda hewani kuanzio leo katika Manispaa ya Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga akikata keki kuashiria kuanza kwa kipindi kipya cha Gold Breakfast baada ya kufanya uzinduzi huo na kuongea na wananchi wa Wilaya ya Kahamakupitia kipindi hicho
***************************
Na Anthony Ishengoma- Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati amesema tayari amekwisha elekeza Manispaa ya Shinyanga na Kahama kutenga maeneo kwa ajili ya kujenga vyuo vikuu katika Mkoa wa Shinyanga.
Dkt.Sengati ameongeza kuwa anataka Mkoa wa Shinyanga kuwa na vyuo vikuu kwasababu yeye kama Muhadhili na Daktari wa falsafa anafahamu vyema mchango wa vyuo vikuu na faida zake kwa maendeleo ya sehemu ambayo kuna vyuo vikuu.
Dkt. Philemon Sengati amesema hayo wakati akiwa katika studio za Radio Gold Fm iliyoko Manispaa ya Kahama alipofika hapo kuzindua kipindi kipya cha Gold breakfast kilichoanza kurushwa leo na radio hiyo ambayo imeanza kurusha matangazo yake kwa siku za karibuni.
Dkt. Sengati ameongeza kuwa atafanya mazungumzo na vyuo vya elimu ya juu kwa lengo la kutaka vyuo hivyo kufungua matawi katika Mkoa wa Shinyanga na kuongeza kuwa Mkoa wa Dodoma umekuwa ukistawi kutokana na uwepo wa Vyuo vingi mkoani humo.
Mkuu huyo wa Mkoa ametoa wito kwa wale wote wanaotaka kuwekeza katika elimu ya juu aje mkoa wa Shinyanga na ardhi kwa ajili ya ujenzi huo inatatolewa bure kwa mwekezaji atakayetaka kuwekeza katika sekta ya vyuo vikuu.
Katika hili tumeona Dododma ikikua kutokana na kuwepo kwa vyuo vikuu vingi, hivyo tunataka kuona Mkoa wa Shinyanga ukistawi kupitia mchango wa vyuo vikuu.
“Binafsi ni nimekuwa Muhadhiri katika chuo Kikuu Dodoma kwa miaka 10 hivyo nitatumia uzoefu wangu kuahakikisha Mkoa unakuwa na vyuo vikuu”. Aliongeza Dkt.Philemon Sengati.
Pamoja na suala la vyuo vikuu Dkt.Sengati pia amezungumzia mchango wa madini kwa Mkoa wa Shinyanga namna ambavyo unachangiwa katika uchumi wa nchi hii na Mkoa wa Shinyanga.
Dkt.Sengati ameliambia radio Gold Fm kuwa Mgodi wa Almadi wa Mwadui sasa unarejesha huduma yake ya kuanza kuzalisha almasi na ifikapo mwezi wa Octoba mwaka huu uzalishaji utakuwa umerejea katika hali yake.
Aidha Dkt. Sengatia ameongeza kuwa kitendo cha mgodi huo kurudi katika uzalishaji ikitaiweka Shinyanga kuwa Mkoa unaoongoza kwa ajili ya utajili wa madini hapa Nchini.
Ikumbukwe kuwa mgodi wa Almasi wa Mwadui ujulikanao Williamson Diamond Mine ulifungwa kufuatia Soko la Almasi Duniani kuporomoka kutokana na mlipuko wa ugonjwa wa Uvico 19 na sasa unarejesha huduma zake.
Kwa upande wa madini ya Dhahabu Dkt. Sengati amesema wachimbaji wadogo kwa sasa wanamchango mkubwa katika uchumi wa nchi akiutaja mgodi mpya unaomilikiwa na wachimbaji wadogo wa Nyandolwa Halmashauri ya Shinyanga kuwa kwa kipindi kifupi umeingiza mapato makubwa serikalini.
Dkt.Philemon Sengati amepongeza uanzishwaji wa Kituo hicho cha Radio na kuwataka kuwa na vipindi vinavyochangia maendeleo ya Mkoa lakini pia kuzingatia maadili ya utangazaji na kuwakumbusha kuwa sekta ya habari ni muhimili wa nne kama ilvyo muhimili ya Bunge na Mahakama.