Na Mariane Mariane Mgombere, Busega-Simiyu
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Busega Bi. Veronica Sayore ameanza zoezi la kutembelea vyanzo vya mapato ya ndani vilivyopo Wilayani Busega, kwa lengo la kuvitambua na kupata uzoefu.
Zoezi hilo limeanza siku ya leo tarehe 11 Agosti 2021 na kusisitiza kwamba atahakikisha anapita kwenye vyanzo vyote vya mapato ya ndani katika Kata zote 15 zilizopo Wilayani Busega.
Aidha, Bi Sayore amesema ni lazima kuwa na tija ya kuongeza ukusanyaji wa mapato ya ndani na kusisitiza kwamba lengo hilo litafanikiwa kwa kuongeza juhudi katika kuchapa kazi. Katika siku ya kwanza Bi. Sayore ameweza kutembelea vyanzo vya mapato yatokanayo na uvuvi, machinjio na mnada, na Stendi ya Wilaya ya Busega. Katika ziara hiyo Bi. Sayore ameambatana na baadhi ya Wakuu wa Idara na Vitengo.