MKURUGENZI wa Jiji la Tanga Sipora Liana akizungumza wakati wa kikao cha Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Jiji hilo leo |
Mstahiki
Meya wa Jiji la Tanga Abdurhaman Shillo kushoto akiteta jambo na
Mkurugenzi wa Jiji la Tanga Sipora Liana wakati wa kikao hicho
Madiwani wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye kikao hicho
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali wakati wa kikao hicho
DIWANI wa Kata ya Msambweni (CCM) Godias Kimath kushoto akifuatilia kwa umakini kikao hicho
wa Idara wa Halmashauri ya Jiji la Tanga wametakiwa kujipima kama
wanatosha kwenye nafasi zao katika kusimamia utekelezaji wa shughuli mbalimbali za maendeleo zinazowagusa wananchi kila siku.
Kauli
hiyo imetolewa na Mkurugenzi wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Spora
Liana wakati wa kikao cha robo ya nne cha Baraza la Madiwani wa
Halmashauri ya Jiji hilo ambapo amewataka watendaji hao kujipima na
kujitathimini kama wanatosha kwenye nafasi zao.
Alisema
kwamba wao watendaji wapo kwa ajili ya kuwawakilisha wananchi hivyo
wahakikishe wanafanya tufanye vitu vya kuwasaidia ili kuweza kukuza
uchumi wao ambao utakuwa chachu ya kuweza kujikwamua kimaendeleo
“Lakini tusisubiri mpaka wananchi waone na waseme kwamba
kweli Halmashauri yao ipo kwa hiyo watendaji na wakuu wa idara kaeni
mkao wa kujipima,je tunatoshaa? waananchi ndio wanaotupima kama tunatosha
au hatutoshi na Mh.Dc yupo hapa kusimamia na kuhakikisha kwamba kila
kitu kinatekelezwa”Alisema Spora
Mkurugenzi
huyo aliongeza kwamba watendaji wapo kuwawakilisha wananchi hivyo ni
muhimu kuona namna ya kushirikiana nao ikiwemo kuwaeleza fursa
zilizopo katika jiji la Tanga ambazo zitawaongezea kipato.
Hata
hivyo alisema lazima waangalia ni namna gani wananchi watatoka hapo
walipo kwa kujiandaa na fursa mbalimbali ikiwemo mradi mkubwa wa Bomba
la Mafuta kutoka Hoima nchini Uganda Hadi Tanga.
Alisema ni muhimu wajue ni vitu gani vitaambatana na bomba la mafuta
vitakavyowasaidia kwenye maeneo yapi watayatumia kuwasaidia wananchi kwa sababu wapo hapo kwa ajili ya wananchi .
Halmashauri ya jiji la Tanga imedhamiria kuongeza ukusanyaji wa mapato na kuibua vyanzo vipya vya mapato.