Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo akipokea Mwenge ikiwa ni ishara ya salamu ya utii ambayo ilifanyika katika viwanja vya shule ya Nia njema na kuhudhuliwa na viongozi mbali mbali wa serikali katika ngazi mbali mbali pamoja na wananchi ambao mwenge huo umeweza kutemnbelea katika miradi 14 yenye thamani ya shilingi bilioni 22.
Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Abdalah wa kushoto akikabidhi ripoti ya salamu ya utii kwa kiongozi wa mbio za Mwenge wa uhuru kitaifa Luteni Josephine Mwambashi.
……………………………………………………………………
VICTOR MASANGU, BAGAMOYO
KIONGOZI wa mbio za mwenge wa uhuru kitaifa Luteni Josephine Mwambashi ametembelea miradi 14 ya maendeleo katika halmashauri mbili za Chalinze pamoja na Bagamoyo zilizopo mkoani Pwani ambapo ameweka mawe ya msingi katika baadhi ya miradi hiyo na mingine kupata fursa ya kuzinduliwa rasmi kwa ajili ya kuanza utekelezaji wake imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 22.
Katika mbio hizo kiongozi huyo alizitaka halmashauri wakiwemo viongozi na watendaji kuhakikisha kwamba wanawashirikisha kikamilifu katika suala zima la miradi mbali mbali kuanzia ngazi za chini hadi za juu ili wananchiw waondokana na hali ya sintofahamu na waweze kujua jinsi ya fedha ambazo zinatengwa na serikali zinavyotumika.
Akiweka jiwe la msingi la mradi wa maji Mlandizi-Mboga ,unaotekelezwa na mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira Dar es salaam(DAWASA) ambao umegharimu kiasi cha bilioni 17 .79, kwa fedha ambazo zimetolewa na serikali.
Katika hatua nyingine kiongozi huyo wa mbioz za mwenge wa uhuru kitaifa alisema kwamba kila mwananchi ana haki ya kujua maendeleo ya miradi hiyo kitokana na fedha ambazo zinatolewa na serikali katika kuleta chachu ya maendeleo.
“Kwanza kabisa kwa upande wangu nimeweza kuionea mradi huu ambao unatekelezwa na DAWASA lakinin pia niwaagize kujenga utaratibu mzuri wa kutoa taarifa kwa watendaji wa ngazi za vijiji, pamoja na ngazi nyingine ili watu wote waweze kuwa na taarifa,”alisema Mwambashi.
Kwa upande wake afisa Mtendaji Mkuu wa DAWASA , Mhandisi Cyprian Luhemeja akitoa taarifa ya mradi huo wa maji anabainisha ujenzi ulianza 2019,umefikia asilimiav95 na zimeshatumika bilioni 13 utakuwa ni mkombozi mkubwa katika kuwaondolea adha ua wananchi kutembe aumbariu mrefu kwa ajili ya kutafuta maji.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Bagamoyo Zainabu Abdalah alifafanua kwamba katika katika Wilaya yake Mwenge huo utaweza kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo 14 ambayo imegharimu kiasi cha shilingi bilioni 22.
Mkuu huyo aliongeza kuwa katika miradi hiyo itahusisha katika sekta ya elimu , afya miundombinu ya barabara, ujarisiamali kwa wanavikundi mbali mbali ikiwemo mradi wa uuzaji wa maziwa, kilimo na bodaboda ambayo itaweza kusaidia kukuza uchumi kwa wananchi.
Awali akipokea mwenge wa Uhuru eneo la Bwawani kutokea Mkoani Morogoro Mkuu wa mkoa wa Pwani, Aboubakar Kunenge alisema mwenge huo ukiwa mkoani humo utakagua,kuweka mawe ya msingi na kuzindua miradi 87 yenye thamani ya bilioni 57.11.5.
Alieleza, utatembelea miradi minne,miradi tisa itawekwa mawe ya msingi,14 itazinduliwa na 60 kukaguliwa kwenye wilaya Saba na halmashauri tisa .
Ukiwa wilayani Bagamoyo, mkuu wa wilaya ya Bagamoyo ,Zainab Abdallah alibainisha mwenge utatembelea miradi 14 ikiwa 7 ni ya kikampeni na mingine 7 ya kimaendeleo,yenye thamani ya bilioni 22.