*********************************
Chuo kikuu cha Ushirika Moshi Tawi la Ruvuma kwa kushirikiana na Tawi la Mtwara wametoa mafunzo kwa Viongozi na Watendaji wa Chama cha Ushirika cha Msingi cha mazao na Masoko Kingerikiti (AMCOS) kilichopo katika Kata ya Kingerikiti Wilayani Nyasa.
Mafunzo hayo ni ya siku 3 yaliyoanza tar.09.08.2021 hadi leo tarehe 11.08.2021 na yanafanyika katika Ukumbi wa Chama hicho ambayo yanalenga kuwawezesha Viongozi na Watendaji wa chama, kuwa na umahiri wa kuandaa mpango wa kibiashara ( Business plan) na Elimu ya Ushirika.
Mkufunzi Evaristo Benitho kutoka Chuo cha Ushirika Moshi, Tawi la Songea amesema amesema mafunzo hayo, yatawasaidia kuandaa Mpango Biashara wa chama na kundaa dira ya Chama, Mikakati na kupata elimu ya Ushirika na kuanzisha miradi na utunzaji na kuimarisha na kuendeleza miradi katika chama chao.
Amefafanua kuwa, katika Dhana ya Ushirika amesema Viongozi na watendaji wamefundishwa kuzitambua fursa zilizopo kwenye Ushirika, namna ya kuyafikia masoko ndani ya mfumo wa Ushirika, umuhimu wa kufanya vikao vya bodi na kufanya na Tathimini na Usimamizi katika Chama chao.
Aisa Ushirika wa Halmashauri ya Wilaya ya Nyasa Menance Ndomba. amesema kwa sasa mafunzo hayo yamefadhiliwa na united States of America development Fund (USADF) na wametoa mafunzo kwa chama hicho, na kila chama cha Ushirika wa Mazao wilayani Nyasa wanatarajia kupata mafunzo hayo ili waweze kuandaa mpango Biashara kwa kuwa na elimu ya Ushirika.
Wakati wa mafunzo hayo washiriki wamepata fursa ya kutembelea na kuona kwa vitendo miradi ya Chama ambayo ni, Mradi wa utoaji huduma za kifedha kupitia NMB wakala, mradi wa mashine ya kuchakataji kahawa (CPU) na Mradi wa kahawa wa wanawake (woman Cofee) ambao una kitalu cha miche ya kahawa ya kisasa kwa ajili ya wanawake tu wa chama hicho.
Mwenyekiti wa washiriki wa mafunzo hayo bi Serafina Mbele amesema mafunzo hayo yamewajengea uwezo wa kuandaa mpango biashara na wataboresha kazi zao kwa kufanya kufuata elimu iliyotolewa kwa kuwa awali walikuwa wakitumia uzoefu.