………………………………………………………..
Na.WAMJW- DSM
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Dorothy Gwajima leo amekutana na Balozi wa Falme za Kiarabu nchini Tanzania (UAE) Mhe. Khalifa Abdulrahman Almarzouqi Kwenye ofisi ndogo za wizara zilizopo jijini Dar es Salaam.
Katika mazungumzo yao wamekubaliana kushirikiana na kubadilishana uzoefu katika kupambana na magonjwa mbalimbali ikiwemo kudhibiti wimbi la tatu la ugonjwa wa Corona nchini.
Dkt. Gwajima amemhakikishia Balozi hiyo utayari wa Wizara yake kushirikiana kwenye maswala yanayohusu uwekezaji kwa upande wa sekta ya afya pamoja na maendeleo kitaifa.