MENEJA wa
Mamlaka ya Mapato nchini (TRA} Mkoa wa Tanga Specioza Owure akizungumza wakati wa kikao cha Wafanyabiashara
MKUU wa Mkoa wa Tanga Adam Malima akifuatilia hoja mbalimbali katika kikao hicho |
Sehemu ya wafanyabiashara wakifuatilia kikao hicho
NA OSCAR
ASSENGA, TANGA
MENEJA wa
Mamlaka ya Mapato nchini (TRA} Mkoa wa Tanga Specioza Owure amesema mamlaka
hiyo imevuka lengo la ukusanyaji wa mapato kwa zaidi ya asilimia 29.7 kwa mwaka
2020/2021.
Specioza aliyasema
hayo wakati akitoa taarifa ya mapato kwa mwaka 2020/2021 na mipango mikakati ya
ukusanyaji mapato waliojiwekea mwaka 2021/2022.
Alisema mamlaka
hiyo mkoani Tanga imefanikiwa kukusanya zaidi ya Sh.Bilioni 154.5 wakati lengo
lilikuwa ni kukusanya Sh.Bilioni 140.2 ambao ni utendaji wa asilimia 110 katika
ya makusanyo hayo.
“Idara ya
Kodi za ndani imekusanya zaidi ya Sh Bilioni 70.5 na Idara ya Forodha
imefanikiwa kukusanya Bilioni 83.99 kwa mwaka 2020/2021 “Alisema
“Lakini kumekuwa
na ongezeko la makusanyo kwa zaidi ya Bilioni 35.3 sawa na asilimia 29.7
ukilinganisha na makusanyo ya kipindi kama hicho kwa mwaka 2019/20 ambapo mkoa
ulikusanya Sh Bilioni 3.99 sawa na asilimia 2.85”Alisema Meneja Owure.
Alizitaja
sababu ambazo ziliwawwezesha kufikia hatua hiyo ya kuvuka lengo kwa mwaka huo
ni kuendelea kuwa na uhusiano mzuri kati yao na viongozi wa mkoa na wilaya zote
pamoja na taasisi zote za Serikali na
walipa kodi.
Meneja huyo
alisema pia lengo la TRA Mkoa wa Tanga kwa mwaka 2021/2022 ni kukusanya zaidi
ya Bilioni 180.88.
Hata hivyo
alisema pia wana mikakati ya kuvuka lengo kwa mwaka huu,TRA imejipanga kufanya
usajili wa wafanyabiashara wapya ambao hawamo kwenye wigo wa kodi.
“Pia tuna
mkakati wa kuendelea kufuatilia na kudai madeni ya kodi kwa ukaribu na kwa
mujibu wa sheria ili kuikomboa kizi hiyo .
Meneja huyo
alisema pia wataendelea kufanya doria kwa kushirikiana na vyombo vya ulinzi na
usalama mkoa ili kuweza kubaini na kuzuia biashara za magendo.