Na Lucas Raphael,Tabora
Watu wawili wa familia moja bibi na mjukuu wake wakazi wa kijiji cha Ibambangulu kata ya Mwatundu wilaya ya Nzega mkoani Tabora wameuwawa kwa kukatwakatwa na mapanga kwa tuhuma za kuuwa watoto 8 wa mke mwenzie kishirikina .
Kamanda wa polisi mkoa wa Tabora Safia Jongo akizumgumza na mwandishi wa gazeti hili alisema kwamba tukio hilio lilitokea Agasti 7 mwaka huu majira ya saa 6;30 usiku katika kitongoji cha Matuli kijjiji cha Ibambangulu kata ya Mwatundu wilaya ya Nzega
Alisema kwamba tukio hilo limeshabishwa na imani za kishirikina baada ya mume kuamua kuwakodi watu na kwenda kuua mke mkubwa kwa tuhuma za kuuwa watoto wa mke mdogo jambo ambalo polisi waendelea na uchunguzi wake
Kamada huyo wa polisi anawataja waliokufa katika tukio hilo ni Nyamizi Ngasa na mjukuu wake Shida Jirangi(11)waliokuwa wamelala pamoja usiku huo.
Alisema kwamba mtuhumiwa wa tukio hilo la mauaji Tuma Manyau aliingia na panga na watu wengine wa kukodiwa na kuanza kumshambulia mke wake huyo alieleza kuwa wakati anamshambulia alikuwa amelala na wajukuu wake wawili na walipoona kitendo hicho walikimbia.
Alisema kwamba baada ya kukamatwa mtuhumiwa alikiri kufanya unyama huo baada ya kwenda kwa mganga ambaye aliwaeleza kuwa mke wake kubwa ndio anawauwa watoto wa mke wake mdogo.
Kamanda Safia alisema kwamba mtuhumiwa alikiri kitendo cha kumuua mjukuu wake ilikuwa ni kuficha ushaidi kwani watoto hao waliona tukio zima la kuuwa kwa bibi yao.
Hata hivyo diwani wa kata ya Mwatundu Paskar Lugonda alisema waliouwawa na bibi Nyamizi Ngasa na mjukuu wake Shida Jirangi(11) ambapo alisema walivamiwa mida ya usiku wa Agost 7 mwaka huu.
Diwani huyo alisema kwamba mtoto moja ambaye alikuwa akipinga kelele na sasa ni marehemu Shida Jiranga kwa lengo la kuomba msaada alifatwa nawatu hao na kushambulia na mapanga hadi akapoteza uhai palepale.
Alisema asubuhi mtoto aliyenusurika na kifo aliwaeleza kila kitu polisi ambao hadi sasa anatunza kwa ajili ya usalama.
Paskar Lugonda alisema anawaomba wananchi wake kuwa na utulivu wakati wa kipindi hiki ambapo jeshi la polisi wilayani nzega linaenendelea na chaanzo cha tukio hilo
Naye Afisa Tarafa wa tarafa ya Nyasa Elikado Komanya akilizungumzia tukio hilo alisema vitendo vya mauaji katika wilaya ya nzega vimeshamiri hasa katika miezi hii ya karibuni na kuwaomba wananchi kushiriki ulinzi shirikishi na kuwataka viongozi wa dini kuimiza amani kwa waumini wao ili kukomesha mauaji wilaya ya nzega.
Kamanda wa Polisi mkoani Tabora Safia Jongo alisema kwamba wanamtunza mtoto huyo kabla ya kuwasiliana na ofisi ya ustwi wa Jamii kwa hatua zingine
Kamanda huyo alisema jeshi hilo linawashikilia watu watano walioshirikia kwenye mauji ya tukio hilo .