Msajili wa Hazina, Mgonya Benedicto (kulia) akipokea nyaraka kutoka kwa aliyekuwa Msajili wa Hazina, Athumani Mbuttuka wakati wa makabidhiano rasmi ya ofisi yaliyofanyika jana katika Ofisi ya Msajili wa Hazina, Dar es Salaam.
Benedicto ameteuliwa na Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa Msajili wa Hazina kuchukua nafasi ya Mbuttuka ambaye ameteuliwa na Mheshimiwa Rais kuwa Mkaguzi wa Ndani Mkuu wa Serikali.
Picha na Ofisi ya Msajili wa Hazina)._