Mabingwa wa Kihistoria Ligi Kuu Tanzania bara timu ya Yanga imezima kelele za watani wao wa jadi Simba baada ya kumtambulisha kiungo wa kimataifa wa Uganda, Khalid Aucho kutoka klabu ya Misr Lel Makkasa SC ya Misri.
Aucho amesaini Mktaba wa miaka miwili kuwatumikia wananchi na kuwa mchezaji mpya wa tano kusajiliwa na Yanga SC.
Baadhi ya wachezaji ambao tayari wameshasajiliwa na kutambulishwa ni Mlinda mlango kutoka nchini Mali, Djigui Diarra kutoka Stade Malien na washambuliaji Wakongo, Fiston Mayele kutoka AS Vita na Heritier Makambo kutoka Horoya ya Guinea pamoja Yussuf Athumani kutoka Biashara United ya Mara.