Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga akizungumza na watumishi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilmali Watu katika kikao kazi cha idara kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa EWURA, jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro akizungumza na watumishi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilmali Watu katika kikao kazi cha idara kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa EWURA, jijini Dodoma.
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Nadhifa Kemikimba akizungumza na watumishi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilmali Watu katika kikao kazi cha idara kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa EWURA, jijini Dodoma.
Watumishi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilmali Watu katika kikao kazi cha idara kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa EWURA, jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Wizara ya Maji, Barnabas Ndunguru akizungumza na watumishi katika kikao kazi cha idara hiyo kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa EWURA, jijini Dodoma.
Mgeni rasmi wa kikao kazi cha Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro akiwa kwenye picha ya pamoja na Madereva wa Wizara ya Maji, jijini Dodoma.
****************************
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, Dkt. Laurean Ndumbaro amesema Serikali inathamini umuhimu na mchango wa kada wezeshi, hivyo hawana budi kujithamini na kuwa watiifu katika utekelezaji wa maelekezo ya Serikali, kuwajibika kwa misingi ya maadili ya kazi kwa watumishi wenzao na wananchi.
Dkt. Ndumbaro ametoa rai kwa watumishi wa Idara ya Utawala na Rasimali Watu Wizara ya Maji kufanya kazi kwa kufuata taratibu, kanuni, sheria na miongozo ya kiutumishi pamoja na kuzingatia misingi ya nidhamu na uadilifu katika majukumu yao ya kiutumishi katika kikao cha viongozi na watumishi wa Idara ya Utawala na Usimamizi wa Rasilimali Watu kilichofanyika Ukumbi wa Mikutano wa EWURA, jijini Dodoma.
Amesema Watunza Kumbukumbu, Makatibu Muhtasi, Madereva na Wahudumu ni kada yenye mchango mkubwa na nafasi kubwa katika taasisi kutimiza malengo yake
kupitia majukumu yao ya kila siku.
Aidha, Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Anthony Sanga amewashukuru watumishi hao na kukiri wamekuwa msaada mkubwa kwa viongozi na wizara kwa ujumla, akisisitiza kuwa anataraji kikao kazi hicho kitakuwa na manufaa makubwa na kuongeza tija katika utendaji wao wa kazi yatakayoleta maendeleo makubwa kisekta.
Mhandisi Sanga amesema kuwa watahakikisha mazingira ya kazi yanaimarishwa, wanasimamia haki za watumishi na kuendelea kutoa motisha kwa wale wote wanaofanya kazi kwa bidii na uadilifu kuthamini mchango wao.
Kikao kazi hicho chenye lengo la kuwajengea uwezo kwenye majukumu mbalimbali.
hicho watumishi wote wa kada za watunza kumbukumbu, makatibu muhtasi, madereva na wahudumu wa Wizara ya Maji na taasisi zake ni cha siku mbili kuanzia tarehe 06-07, Agosti kikiwa kimebeba kaulimbiu ya Nidhamu, Uadilifu na Uwajibikaji ni Chachu ya Huduma Bora.