***********************************
Na Mwamvua Mwinyi,Mafia
WILAYA ya Mafia mkoani Pwani,imepokea chanjo ya UVIKO 19 zipatazo 1,000 ambazo zitasaidia kujikinga na ugonjwa huo.
Mkuu wa wilaya hiyo ,Mhandisi Martin Ntemo amepokea chanjo katika uzinduzi wa utoaji wa chanjo hiyo kiwilaya na kuchanja kwa hiari yake.
Baada ya kuchanja ,Ntemo alieleza chanjo zilizopolelewa kwa awamu ya kwanza zitaanza kutolewa kwa wauguzi na watoa huduma wa afya.
Alisema kwamba,pia watapatiwa watu wenye umri zaidi ya miaka 45 wenye changamoto ya maradhi ya muda mrefu, watumishi wa umma,wahudumu katika mahotel na migahawa,na wazee.
Maeneo yatakayotoa huduma hii ni hospital ya wilaya, pamoja na zahanati ya Baleni,Utende,Bweni,Chemchem na Kirongwe.
Ntemo aliwahamasisha wananchi kujitokeza kuchanja chanjo hiyo itakayowasaidia na kuwaomba wapuuzi uzushi wowote juu ya chanjo hiyo.
“Licha ya kuwa ni kinga lakini pia itapunguza makali ya homa ya ugonjwa huu na vifo vinavyotokana na Uviko.