Mwenyekiti wa vituo vyote Kanisa Halisi la MUNGU BABA Ndani na Nje ya Nchi ya Tanzania, BABA Halisi akizungumza jijini Dar es Salaam katika Ibada maalumu ya kufuta mapatilizi yaliyokuwa bado yanaifutikia Nchi ya Tanzania.
…………………………………………………………
NA NOEL RUKANUGA, DAR ES SALAAM.
Kanisa Halisi la MUNGU BABA limefanya ibada maalum ya kufuta mapatilizi yaliyokuwa bado yanaifuatilia nchi ya Tanzania pamoja na kumuombea Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassani ili kumuepusha na changamoto mbalimbali katika utekelezaji wa majukumu yake.
Kanisa hilo limekuwa likiunga mkono shughuli, sera na maadhimio mbalimbali yanayopitishwa na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania likiwa sehemu ya jamii pamoja na kueendelea kutoa ushirikiano wake kwa Taifa.
Akizungumza hivi karibuni katika ibada maalumu ya kufuta mapatilizi yaliyokuwa bado yanaifuatilia nchi ya Tanzania, iliyofanyika Makao Makuu ya Kanisa la MUNGU BABA jijini Dar es Salaam, Mwenyekiti wa Vituo vyote vya Kanisa hilo Ndani na Nje ya nchi ya Tanzania, BABA Halisi, amesema kuwa taifa la Tanzania linatakiwa kuendelea kumtegemea Mungu wakati wote.
BABA Halisi amesema kuwa kuna mambo makubwa yametokea nchini Tanzania baada ya sauti ya chanzo cha mema kuwepo ikiwemo amani imetawala kwa wote waliowaombewa katika kanisa hilo, matatizo kuondoka pamoja wale waliokuwa na magonjwa magumu wamepona.
“Tunawatenga viongozi wote na mashimo ambayo wamewekewa barabarani na kumuinua Rais Samia Suluhu Hassani kwa Shukrani, dua na maombi ili MUNGU BABA ambaye ni chanzo amlinde na kumtetea katika majukumu yake ya kila siku”
Kanisa hilo limekuwa likiendesha Ibada na maombi kila iitwapo leo ambapo katika maombi, dua na shukrani hujielekeza ama hulinyenyekeza Taifa kwa MUNGU BABA ili aendelee kulilinda pamoja na viongozi wake akiwemo Mhe. Rais Samia Suluhu Hassani.
Kanisa hilo limekuwa na mchango kubwa kwa Taifa la Tanzania kwani tokea kuanzishwa kwake limefanya mambo kaza wa kaza katika huduma za jamii ikiwemo sekta ya Afya, Elimu, Miundombinu lakini pia katika kuombea amani ya nchi hii ambayo ni muhimu kuliko kitu chochote kile.
Kanisa hilo limejizolea umaarufu mkubwa Afrika Mashariki ambako kote lina vituo na kutapakaa duniani kote ambako makuhani wenyewe wanapoiskia Sauti ya Chanzo tu kupitia BABA Halisi hawafanyi ajizi hulianzisha Kanisa.
Kanisa limekuwa likifundisha mafundisho ya ibada ni uzalishaji na upendo usiobagua na kutojihusisha na masuala ya kisiasa bali hushirikiana na wanasiasa pale Kanisa linapohitaji huduma inayohusiana na siasa, lakini pia pale wanasiasa wanapohitaji mchango wa Kanisa hilo kwani serikali haina dini.
Hata hivyo BABA Halisi anawakaribisha watu wote kutoka Mataifa mbalimbali kwa ajili ya huduma za maombezi, ushauri na kiroho kanisa hilo halina masharti yoyote dini,makabila na Mataifa yote mnakaribishwa poopte nchini.
Kanisa halisi la MUNGU BABA lakini hata mikoani na Mataifa mbalimbali ikiwemo Afrika Mashariki na nchi za Kusini mwa Afrika Zambia, DR Kongo, Msumbiji na kwingineko kwa Dar es Salaam Makao Makuu yake yapo huko Tegeta Namanga