KATIBU
Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wilfred Kidau akizungumza na
waandishi wa Habari leo kuhusu kuelekea mkutano huo
MGOMBEA Urais wa Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) Wallace Karia akizungumza na Waandishi wa Habari leo |
NA OSCAR ASSENGA,
TANGA
KATIBU Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wilfred
Kidau amesema mkutano mkuu wa Kawaida wa Shirikisho ambapo moja ya agenda kubwa ni Uchaguzi Mkuu unatarajiwa
kufanyika Jijini Tanga kesho
Ambapo
maandalizi yake yakiwa yamekamilika kwa asilimia 95 ya wageni
mbalimbali wakiwemo wa Kimataifa kutoka Shirikisho la Soka Barani Africa
CAF na Shirikisho la Soka Duniani FIFA wakitarajiwa kuhudhuria mkutano
huo
Mkutano huo unatarajiwa kufanyika kwenye Ukumbi wa Hotel ya
Tanga Beach Jijini hapa huku asilimia 5 ya wajumbe iliyobakia ikitarajiwa
kuwasili leo kuungana na wenzao kwa ajili ushiriki wao.
Akizungumza na waandishi wa Habari leo Jijini Tanga Katibu wa
Shirikisho la Soka nchini Tanzania (TFF) Wilfred Kidau alisema kwamba
maandalizi yamekamilia huku wageni mbalimbali wakiwasili ikiwemo Rais wa Shirikisho
la Soka nchini Somalia ambaye pia vilevile ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya
CAF.
Alisema pia walikuwa na kamati ua uchaguzi wa TFF
kuhakikisha maandalizi ya muhimu yanakamilika wao kama sekretarieti ni wajibu
wao kuhakikisha kamati ya uchaguzi ili iweze kufanya mambo yake kwa asilimia
mia moja.
Alisema wapo wageni wengine mbalimbali wameanza kuwasilia Jijini
Tanga ambapo wegine wa Kimataifa kutoka Shirikisho la Soka Duniani (FIFA) na
Kutoka Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) wakiwemo wajumbe wawili wawili
wapo njiani tayari kutua Jijini Tanga.
Awali akizungumza na waandishi wa Habari Mgombea Urais wa
Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) Wallace Karia alisema kikatiba kila baada ya
miaka minne wanafanya uchaguzi na wa mwisho ulifanyika mwaka 2017 na safari hii
wanafanya AgostI 7 wanafanya uchaguzi huo hapa jijini Tanga huku akiwaomba
watanzania wawaombee kwa ajili ya mkutano huo.
Alisema kwamba mkutano
huo utajadili taarifa zao za utekelezaji za mwaka na yeye atatoa taarifa yake
ya miaka minne ya uongozi wake na wajumbe watajadili na baadae ya hapo wataenda
kwenye uchaguzi huo anamshukuru Mwenyezi Mungu kwenye mkutano huo mgombea wa
Urais atakuwa pekee yake na uthibitisho utafanyika kwenye mkutano huo hivyo
anaomba wajumbe waweze kunithibitisha.
Naye kwa upande wake Mwenyekiti wa timu ya Biashara United
ya Mara Selemani Mataso alisema uchaguzi huo ni muhimu sana hasa wao viongozi
wa vilabu wanahitaji kupata watu ambao watawasaidia kuhakikisha wanaenda
kutengeneza muonekano wa mpira ambayo haiwezi kuwa na shida na kuweka usawa wa
vilabu vya ligi kuu na ligi daraja la kwanza.
Alisema wakipatikana viongozi namna hiyo wakuangalia maslahi
ya mpira inakwenda kutengeneza safu ya kuonyesha kwamba soka linakuwa
linakwenda kujipambanua kuendesha soka la kisasa.