****************************
NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM
Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya FURAHIKA EDUCATION TANZANIA Bw. David Msuya amewataka Watanzania kumuunga mkono Rais Mheshimiwa Samia Suluhu kwa kujiokeza kwa wingi kwenye vituo vya afya kwaajili ya kupata chanjo ya kujikinga na UVIKO 19.
Ameyasema hayo leo Bw.Msuya baada ya baadhi ya watu kujitokeza katika mitandao ya kijamii na kuanza kuikosoa chanjo ambayo wataalamu wa afyya wameshajiridhisha na kutamka kuwa chanjo hiyo ni salama.
“Watanzania tusipende kusikiliza yanayosemwa mitandaoni na watu ambao wameamua tu kukosoa mambo ambayo ni muhimu hasa kwa taifa letu, kuna wengine wanasema chanjo hii inamadhara kwenye suala la uzazi (Ngvu za kiume), kuna wengine wanaijaji na kusema ni hatari baada ya miaka kadhaa, haya yote ni uafanya watanzania wasiweze kupata chanjo, niwasihi Watanzania wenzangu tujitokeze kwa wingi kupata chanjo”. Amesema Bw.Msuya.
Aidha Msuya amesema kuna ulaimu wa wataalamu wa vituo vya kutolea chanjo waongezeke ili kwenda na kasi kwasababu watu wameshakuwa ni wengi kwenye vituo hivyo.
Pamoja na hayo Bw.Msuya amesema wanafanya majadiliano na Chama cha Netball Taifa kuona ni namna gani wanaweza kudhamini mashindano ya Taifa ya Netball kwa kuweka fedha kiasi cha shilingi Milioni 150.
“Kumekuwa na changamoto ya wadhamini katika mashindano ya Netball Taifa yamekuwa yanaendeshwa kwa kusuasua na kama mazungumze yetu sisi na viongozi wa Serikali na vyama husika tunataka kudhamini kwa Milioni 150 mashindano ya kitaifa ambayo tutakuwa tunayasimamia na kutoa zile zawadi”. Amesema