Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka Wizara Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto ,Dk Saitore Laizer,akizungumza wakati akifungua warsha ya wadau wa macho iliyofanyika leo Agosti 4,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka Wizara Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto ,Dk Saitore Laizer,akisisitiza jambo kwa washiriki wa warsha ya wadau wa macho iliyofanyika leo Agosti 4,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Dk. Ntuli Kapologwe,akizungumza wakati wa warsha ya wadau wa macho iliyofanyika leo Agosti 4,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi wa Mafunzo kutoka Wizara Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto,Dkt.Fadhili Lyimo,akizungumza wakati wa warsha ya wadau wa macho iliyofanyika leo Agosti 4,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Msaidizi Kitengo cha Magonjwa yasiyoambukiza Dkt.James Kihologwe,akizungumzia jinsi walivyojipanga kupata maoni mapya wakati wa warsha ya wadau wa macho iliyofanyika leo Agosti 4,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la sightsavers Tanzania Bw.Godwin Kabalika,akielezea jinsi walivyoshiriki katika warsha ya wadau wa macho iliyofanyika leo Agosti 4,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakifatilia mada mbalimbali zilizokuwa zikitolewa wakati wa warsha ya wadau wa macho iliyofanyika leo Agosti 4,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka Wizara Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto ,Dk Saitore Laizer,akiwa katika picha ya pamoja na washiriki mara baada ya kufungua warsha ya wadau wa macho iliyofanyika leo Agosti 4,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………………………………………
Na Alex Sonna,Dodoma
WIZARA ya Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto imesema imejipanga kubadilisha mitaala mipya ya kufundishia masomo ya macho lengo likiwa ni wanafunzi wa ngazi za chini wanaosoma masomo hayo waweze kutambulika.
Hayo yameelezwa leo Agosti 4,2021 na Mkurugenzi wa Mafunzo kutoka Wizara hiyo,Dk Saitore Laizer wakati akifungua warsha ya wadau wa macho.
Dk.Laizer amesema kuwa lazima ifike mahali kuwe na mitaala hai ili wanafunzi wa ngazi mbalimbali watakapomaliza waweze kutambulika.
“Nategemea sana tujadiliane kwa pamoja kuhusu kuikataa hii hali ambayo inatokea sasa hivi,mimi nawaza lazima ifike mahali kuwe na mitaala hai ili wanawafunzi watakapomaliza waweze kutambulika.Inshu ya mitaala hatuwezi kuikwepa lakini kuna vyuo ambavyo vilikuwa vinatoa mafunzo miundombinu yao ni mibovu hivyo ni lazima tuikarabati pamoja na kuiongeza,”amesema Dk.Laizer .
Amesema mara baada ya maboresho katika vyuo hivyo,ni lazima kuwe na vifaaa vya kujifunzia na kufundishia na maabaara kwa ajili ya kuwajengea uwezo wanafunzi huku akisisitiza ni lazima walimu wajengewe uwezo.
“Tutahitaji kufanya utafiti utakaotuongoza katika matibabu ya sasa eneo hili hatuwezi kulikwepa tunaweza kutengeneza tafiti za hapa kwetu na watu wa kufanya utafiti wapo wengi lakini wakati mwingine wanashindwa kuridhisha tupate trend ya magonjwa yanayosumbua.
“Nguvu zote za pamoja hazitatuangusha kwa umoja wetu tukiungana nauhakikishia tunaweza kuushika mkono kwa pamoja tukauhamisha kwingine hili la macho ni kamlima kadogo .Tukumbuke huduma zinazidi kuwa nyingi ila tulikuwa tumelala,”amesema.
Aidha,amewashukuru wadau kwa jinsi ambavyo wameisadia Wizara katika kununua vifaa huku akisisitiza kile ambacho wanakitaka ndicho ambacho wadau wamekifanya.
“Kuna baadhi huwa wanakuja na kitu ambacho hujawahi kukisikia ila wanataka kukichomeka hao huwa nawatoa nje hii ndio njia nzuri ya kuipeleka Nchi katika hili lazima mdau aje tukae tumuoneshe maeneo yetu ya kipaumbele,”amesema.
Hata hivyo,Dk.Laizer amesisitiza umuhimu wa wataalamu kuendelea kuulinda uoni ambapo amedai asilimia 80 ya matatizo ya macho yanaweza kuzuilika.
“Tukumbuke wapo ambao huoni wao haupo kama wakwetu na akitaka kutoka lazima ataomba msaada kuna wengine uoni wao ni hafifu na kuna wengine hawaoni kabisa tujaribu kutafakari asilimia 80 ya vinazulilika sasa kama vinazuilika na Tanzania lazima kama Nchi tujiulize sababu ni nini katika kikao cha leo tupo kutafakari kama kuna zuilika kwanini tunashindwa kikao hicho ndio kitatupa mbinu,”amesema.
Dk.Laizer amesema visababishi vya uoni hafifu ni pamoja na huduma za afya ambazo haziridhishi hapa nchini ambapo amedai sababu ni wataalamu wachache katika sekta ya afya.
“Vyuo vinavyozalisha wataalamu wa afya kwa sasa wataalamu wamepungua mahitaji yanaongezeka lakini mahitaji yapo pale pale wataalamu wa macho Tanzania ni asilimia 38 ndio waliopo 62 hawapo Hizi takwimu hazikubaliki.
“Watanzania wengi wanaonwa katika ngazi ya awali hatuna Diploma yoyote ya macho inayozalishwa hapa Kwa kusinzia kwetu hapa tunaumia sana hata kwenye Hospitali za Wilaya hawapo kabisa na kwenye Hospitali ya Rufaa wanahesabika kabisa huku chini kuna shida lakini wataalamu ni wachache.
“Tumekusahau kule tulikotoka tunawafundisha wataalamu wa juu huku chini kuna shida,tutafakari tumejikwaa wapi na changamoto ni nini nikijaribu kutafakari mojawapo ya shida elimu yetu imebadilika kuanzia 2005 mambo mengi yamebadilika.
“Watalaamu wenye Diploma walikuwa hawatambuliki hiyo ikawaudhi watu kwani haitambuliki Serikali hii ilikwaza watu ilifanya watu wakakacha kujiunga katika hivyo vyuo,”amesema.
Kwa upande wake,Mkurugenzi wa Huduma za Afya,Ustawi wa Jamii na Lishe kutoka Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa,(TAMISEMI) Dkt Ntuli Kapologwe amesema kikao hicho ni cha mustakabali wa sekta ya macho hivyo Ofisi yake inajukumu la utekelezaji wa sera na utekelezaji wa sera hutegemea uwe na watu sahihi.
“Sisi tutashiriki viliyo katika kikao hichi na sisi Tamisemi tutaenda kuyatafrisi na kuandaa plan katika maeneo mbalimbali tunaishukuru Wizara ya afya na wadau wote ambao wamewezesha,”amesema.
Kwa upande wake Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la sightsavers Tanzania Bw.Godwin Kabalika, amesema wanapenda kuishukuru Serikali kwa jinsi ambavyo imeendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa sekta ya macho.
“Sisi kama wadau tupo tunajali sana ushirikiano na Serikali na hatuwezi kwenda mbele bila Serikali na leo imedhihirisha hilo,kwa niaba ya wadau wote tunapenda kuishukuru Serikal,”amesema.