Na Mwamvua Mwinyi,Pwani
Mkuu wa mkoa wa Pwani,Aboubakar Kunenge aamuru watuhumiwa 10 waliokaidi katazo la Mahakama kukamatwa na kuhojiwa, akiwemo mwenyekiti wa CCM Kata ya picha ya Ndege Godfrey Mwaipopo.
Kunenge amefikia uamuzi huo wakati alipokutana na Wananchi wa Lulanzi kata ya Picha ya Ndege Kibaha kutatua kero ya Mgogoro wa Ardhi shamba na 16 kati ya Wananchi na mmiliki Ndugu yesalm Said Bin kleb.
Pamekuwepo na Uvamizi katika shamba Na 16 lilipo Lulanzi Kibaha na Mgogoro huo umeshughuliwa Ngazi ya Wilaya Mkoa na Wizara, na sasa upo mahakamani.
Kunenge aliwataka Wananchi hao kuheshimu sheria na katazo la mahakama ,amesema kukiuka huko kuna hatarisha Usalama amani na utuluvi eneo hilo.
“Vishoka na Matapeli wa Ardhi Pwani si salama kwao, kazi yangu ni kutenda haki, kama serikali ina haki ipate haki yake, kama Mwekezaji ana haki apate haki yake, kama Mwanachi anahaki apate haki yake, Hakuna atakayeonewa. Unaeneo lako una hati yako sitaruhusu mtu aingilie eneo lako, alisisitiza Kunenge.
Kunenge aliwachukulia hatua majina 10 ya Matapeli wa Ardhi wanaoendelea kuuza Ardhi katika Eneo hilo licha ya kuwepo katazo la Mahakama kwa kumtaka Mkuu wa Kituo cha Polisi Kibaha kuwachukua watuhumiwa hao na kuwahoji.