………………………………………………………………………..
Na Silvia Mchuruza,Kagera,
Ni katika uzinduzi wa chanjo ya kuzuia maambukizu ya homa kali ya mapafu corona mkoani kagera katika hospitali ya mkoa katibu tawala wa mkoa wa kagera profesa Faustin Kamzora ambae alikuwa rasmi amewataka wananchi kutokuwa na wasiwasi jui ya chanjo hiyo.
Akizungumza na wananchi pamoja na watumishi wa afya katika ukumbi wa hosptal hiyo amesema chanjo hiyo ni muhimu kutolewa kwa makundi yaliyotajwa hasa wazee wenye umri wa miaka 50 na kuendelea pamoja na watu walio katika makundi maalumu.
Hata hivyo ameongeza na kuwataka viongozi wa dini kuwahasisha wananchi kuchoma chanjo hiyo ambapo halmashauri zote 8 za mkoa wa kagera zimeishapokea chanjo hizo na vito vitakavyotumika kutoa chanjo hizo katika halmashauri zote ni vituo 18.
Pia amesema kuwa katika halmashauri ya bukoba manispaa vituo vitakavyotumika kutoa chanjo hiyo ni 2 ambavyo ni hospital ya rufaa ya mkoa na hospital ya wilaya zamzam ambapo amewataka hata wananchi kutokuwa na tabia ya kurundikana maenwo ya msibani.
“Maeneo ya misibani ndo sehemu ambazo kwa sasa zinaonekana kuwa chanzo cha kuenea kwa UVIKO 19 kwo nawaomba wananchi tuachane na tamaduni zetu ili kujilinda na janga hili”
Nae askofu wa jimbo katoriki la bukoba Methodius Kilaini amezidi kuwaimiza watumishi wa dini wenzake kuzidi kutoa wito na kuwataka hata waumini kuzingati chanjo hiyo kuwa ni muhimu zaidi hasa wazee walio katika umri wa zaidi ya miaka 50.
“Kwa sasa tunazidi kuwaimiza wananchi hata katika ibada zetu ili kujikinga na ugonjwa huu maana tusipojikinga mapema tutapata shida sisi wenyewe”
Sambamba na hayo wananchi wametakiwa kutoogopeshana juu chanjo kwani chanjo ni salama na aina madhara yoyote.