Mwenyekiti wa Taasisi ya Mzalendo Foundation, Khamis Mgeja akizungumza muda mfupi baada ya kupata chanjo dhidi ya Uviko- 19 jana.Picha na Baltazar Mashaka
Mgeja ambaye ni Mwenyekiti wa CCM mstaafu wa CCM Mkoa wa Shinyanga, alitoa ombi hilo wakati akihojiwa kwa njia ya simu jana baada ya kupata chanjo ya Uviko 19.
Alisema wapotoshaji wa chanjo ya Uviko-19 ni sawa na magaidina upotoshaji huo ni aina mpya ya ugaidi hivyo serikali isiwafumbie macho badala yake iwachukulie sawa na wahalifu wengine.
“Kama unazuia watu wasichanjwe maana yake unataka wafe, kwa hiyo hawa ni sawa na magaidi,wanaopotoshaji hao dhidi ya chanjo ya Uviko-19 wachukuliwe sawa na wahalifu wengine, hao ni sawa na wauaji wa Kimbari hivyo wachukuliwe hatua za kisheria, tusiwachekee kwani ukicheka na nyani utavuna mabua,”alisema Mgeja.
Mwenyekiti huyo wa Mzalendo Foundation alisema kuwa taaluma ya kitaalamu inakosolewa kitaalamu siyo kuingiza siasa na upotoshaji, watu hao wanaopinga chanjo ya Uviko-19 ni bora wakae kimya au watupe mbadala wa chanjo hiyo kuliko kuwapotosha watu.
“Ninampongeza Mhe. Rais Samia Suluhu kwa kukubali Watanzania wapatiwe chanjo dhidi ya Uviko-19, binafsi nimejitokeza kuwa miongoni mwa Watanzania wa mwanzo kabisa kuchanjwa chanjo hii dhidi ya Uviko-19,”alisema Mgeja na kuwaomba wananchi wengine wajitokeze kuchanjwa.