- Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akizungumza na Mkurugenzi wa Kampuni ya China First Highway Engineering Ltd nchini, Weipeng Ju katika kikao kilichofanyika katika ofisi za Wizara ya Maji, Mtumba, jijini Dodoma.
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akiwa kwenye picha ya pamoja na viongozi wa Kampuni ya China First Highway Engineering Ltd.
****************************
Waziri wa Maji, Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amekutana na Wakandarasi wa Kampuni ya China First Highway Engineering Ltd na kufanya nao mazungumzo kuhusu utekelezaji wa miradi ya maji nchini katika ofisi za Wizara ya Maji, Mtumba, jijini Dodoma.
Waziri Aweso amekutana na viongozi wa Kampuni hiyo Mkurugenzi wa Kampuni ya China First Highway Engineering Ltd nchini, Weipeng Ju na Meneja Biashara, Guanghui Wei na kujionea kazi zilizofanywa na zinazoendelea kufanywa na kampuni hiyo maeneo mbalimbali duniani.
Mhe. Aweso alidhirishwa na uwezo wa kampuni hiyo na kusema kuwa watakaa chini pamoja kama wizara na kufanya uchunguzi wa kina kuhusu kampuni hiyo na kuona kama kuna uwezekano wa kufanya nayo kazi hususani kwenye miradi ya kipaumbele kama kutoa maji Ziwa Victoria na kuyaleta Dodoma.
Mkurugenzi wa Kampuni hiyo nchini Tanzania, Weipeng Ju amesema kampuni yao ni miongoni mwa kampuni 10 bora nchini China na wako tayari kufanya kazi na Wizara ya Maji kwa kutekeleza mirai ya maji tente bora.
Kikao hicho na kampuni hiyo ni hatua ya Serikali kuhakikisha namna ya kufikisha huduma ya maji nchi nzima kwa kutumia wakandarasi wenye uwezo.