Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akizindua Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA katika Halmashauri ya Wilaya ya Busokelo, wakati wa ziara yake ya kikazi Mkoani Mbeya. Kushoto ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (Mb.), Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb.).
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akisikiliza taarifa ya mradi wa Chuo hicho cha Ufundi Stadi kutoka kwa Mkurugenzi Mkuu wa VETA, Dkt. Pancras Bujulu (wa pili kutoka kushoto). Kulia ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama na Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Mhe. Prof. Joyce Ndalichako (Mb.).
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama na Viongozi wengine wakipata maelezo ya namna ya ushonaji wa nguo kutoka kwa mmoja wa wanafunzi wanaofadhiliwa na Serikali kupitia Mafunzo ya Uanagenzi yanayoratibiwa na Ofisi yake katika Chuo cha Ufundi Stadi cha VETA katika Wilaya ya Busokelo.
Waziri Mkuu, Mhe. Kassim Majaliwa akifafanuliwa jambo na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Sera, Uratibu, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Mhe. Jenista Mhagama (kushoto) alipotembelea karakana ya wanafunzi wa fani ya Useremala wanaofadhiliwa na Serikali kupitia Mafunzo ya Uanagenzi. Kulia ni Naibu Spika wa Bunge, Mhe. Dkt. Tulia Ackson na Mkuu wa Mkoa wa Mbeya, Juma Homera.
Sehemu ya wanafunzi wa fani ya Umeme wa Majumbani wanaofadhiliwa na Serikali kupitia Mafunzo ya Uanagenzi. yanayoratibiwa na Ofisi ya Waziri Mkuu wakiwa katika masomo yao ya Vitendo ikiwa ni sehemu ya kuwajengea ujuzi.
PICHA ZOTE NA OFISI YA WAZIRI MKUU
(SERA, URATIBU, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU)