*********************************
Jengo la Kituo Cha kupokea, kupoza na kusambaza umeme kilichopo Msamvu mkoani Morogoro kikiteketea kwa moto na kusababisha umeme kukatika mji mzima.
……………………………………
NA FARIDA SAIDY,MOROGORO.
Kufutia moto uliozuka katika jengo la kuthibiti mfumo wa upande wa umeme msongo wa Kilovoti 33 la kituo cha kupozea na kusambaza umeme cha msamvu manispaa ya Morogoro na kusababisha Mkoa Morogoro kukosa huduma ya umeme kwa muda usio julikana Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Bwana Martin Shigela amesema ataunda tuma ya kuchunguza chanzo cha moto huo.
Shigela ameyasema hayo mara baada ya kufika eneo la tukio na kujione madhala yaliojitokeza katika kituo hicho ambapo mpaka sasa chanzo cha moto huo hakijajulikana.
Aidha amesema kuungua kwa kituo huicho kumeleta madhala makubwa kwa shirika la umeme nchini,Viwandani,wafanyabishara na wananchi wa mkoa huo kwa ujumla,ambapo serikali kwa kushirikiana na TANESCO itahakikisha huduma ya umeme inarejea kwa haraka.
Kwa upande wake meneja wa TANESCO Mkoa wa morogoro Mhandisi Fedgrace Shuma amewatoa hofu wakazi wa Mkoa wa Morogoro kuwa huduma ya umeme italeja ndani ya masaa 12.
Aidha amesema mitambo yote iliyomo ndani ya jengo lililoungua ipo salama isipo kuwa sehemu ya kuthibiti mfumo wa umeme ndio iliyoathilika zaidi na kusababisha kituo hicho kushindwa kufanya kazi .
Mhandisi shuma ameongeza kuwa waatalam na mafundi wa Tanesco wanaendela na kazi ya kuhakikisha huduma ya umeme inarejea kwa haraka iwezekanavyo.
Nae Kamanda wa jeshi polisi Mkoa wa Morogoro ACP Photnatuc Musilm amesema jeshi la polisi kwa kushirikiana na vyombo vingine vya ulizi vikiwemo,jeshi la zima moto na uokoaji na jeshi la kikosi cha mzinga katika kuhakikisha hali ya usalama inaimarika katika eneo la tukio.
Akizungumza mara baada ya zoezi la uzimaji wa moto Mkaguzi wa jeshi la zima moto na uokoji mkoa wa Morogoro Afande Neema Leonard Msolwa amesema bado chanzo cha moto huo hakijafahamika wanaendelea na uchunguzi wa chanzo hicho.