Home Mchanganyiko TANZIA:WAZIRI KWANDIKWA AFARIKI DUNIA

TANZIA:WAZIRI KWANDIKWA AFARIKI DUNIA

0

Mbunge wa Jimbo la Ushetu mkoani Shinyanga, ambaye pia ni Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Elias Kwandikwa amefariki Dunia.

Kwa mujibu wa taarifa kutoka chanzo cha uhakika, Kwandikwa amefariki jijini Dar es Salaam leo alipokuwa akipatiwa matibabu.

Katibu wa Mbunge huyo ndugu Julius Lugobi, ameithibitishia taarifa ya kifo cha Kwandikwa.

Kwandikwa aliwahi kuwa Naibu Waziri wa kazi.

Alizaliwa Julai mosi mwaka 1966 na hivyo amefariki akiwa na umri wa miaka 55.