*******************************88
– Ataka Wamiliki na LATRA kusimamia level seat na abiria wote kuvaa Barakoa.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Mhe. Amos Makalla ametoa tamko la Kusisitiza matumizi sahihi ya Barakoa kwa kila abiria wote wanaopanda kwenye vyombo vya usafiri huku akiwataka Wamiliki wa Vyombo hivyo kuwaelekeza madereva na makondakta kuepuka kubeba abiria asiavaa Barakoa.
RC Makalla ametoa msisitizo huo wakati wa kikao Cha Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa kilichoketi kupitia tathimini ya utekelezaji wa mwongozo ukiotolewa na Wizara ya Afya juu ya kujikinga na Corona na kuendelea kusitiza Suala la level seat.
Mhe. Makalla amesema kumekuwa na ulegevu wa usimamizi kwenye baadhi ya maeneo ambapo ametoa maelekezo kwa Jeshi la Polisi, Wakuu wa Wilaya na LATRA kuhakikisha wanasimamia ipasavyo mwongozo wa Wizara ya Afya.
Kutokana na changamoto za usafiri kwa wanafunzi, RC Makalla ameruhusu Daladala kubeba Wanafunzi watano watakaosimama lakini kwa kigezo Cha wanafunzi hao kuwa wamevaa Barakoa.
Aidha RC Makalla ameendelea Kusisitiza Wananchi kuepuka Mikusanyiko isiyokuwa na lazima na Kama ikitokea Kuna ulazima taratibu zote za kujikinga zizingatiwe.
Kuhusu suala la Chanjo RC Makalla amefurahi kuona Wananchi wamekuwa na mapokeo makubwa ya kupokea chanjo ambapo kwa Mujibu wa Mganga mkuu wa Mkoa huo adi kufikia Jana tayari Wananchi 10,000 wamefanya booking na wanahofia Chanjo zitawahi kumalizika.