Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TAA) Bw.Hamza Johari akizungumza katika hafla ya kusaini mikataba mitatu ya ushirikiano kati ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) , MS-TCDC na LHRC leo katika Chuo hicho Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji Prof. Zacharia Mganilwa akizungumza katika hafla ya kusaini mikataba mitatu ya ushirikiano kati ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) , MS-TCDC na LHRC leo katika Chuo hicho Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa Programu MS-TCDC, Bi.Sara Teri akizungumza katika hafla ya kusaini mikataba mitatu ya ushirikiano kati ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) , MS-TCDC na LHRC leo katika Chuo hicho Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi wa kituo cha LHRC Bi.Anna Henga akizungumza katika hafla ya kusaini mikataba mitatu ya ushirikiano kati ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) , MS-TCDC na LHRC leo katika Chuo hicho Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT),Prof. Zacharia Mganilwa(kulia) akiwa pamoja na Mkurugenzi wa Programu MS-TCDC, Bi.Sara Teri (kushoto) wakisaini mikataba ya ushirikiano kati ya Chuo cha NIT , MS-TCDC na LHRC leo katika Chuo hicho Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT),Prof. Zacharia Mganilwa(kulia) akibadilishana mikataba na Mkurugenzi wa Programu MS-TCDC, Bi.Sara Teri (kushoto) katika hafla ya kusaini mikataba mitatu ya ushirikiano kati ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) , MS-TCDC na LHRC leo katika Chuo hicho Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT),Prof. Zacharia Mganilwa(kulia) akiwa na Mkurugenzi wa Programu MS-TCDC, Bi.Sara Teri (kushoto) wakionesha mikataba waliosaini katika hafla ya kusaini mikataba mitatu ya ushirikiano kati ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) , MS-TCDC na LHRC leo katika Chuo hicho Jijini Dar es Salaam
Mkuu wa Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT),Prof. Zacharia Mganilwa(kulia) akiwa na Mkurugenzi wa kituo cha LHRC Bi.Anna Henga (kushoto) wakionesha mikataba waliosaini katika hafla ya kusaini mikataba mitatu ya ushirikiano kati ya Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) , MS-TCDC na LHRC leo katika Chuo hicho Jijini Dar es Salaam
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TAA) Bw.Hamza Johari akipata picha ya pamoja na viongozi wa taasisi hizo zilizoingia makubaliano.
(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)
**********************
Chuo cha Taifa cha Usafirishaji (NIT) kimeingia makubaliano ya ushirikiano na taasisi mbili ikiwemo Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC) na taasisi inayojihusisha na utoaji wa elimu katika masuala ya uongozi MS TCDC ili kuboresha utendaji wa Chuo.
Akizungumza katika hafla hiyo Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usafiri wa Anga nchini (TAA) Bw.Hamza Johari amesema ushirikiano huo utazidi kukiboresha Chuo hicho na kukiwezesha kutimiza malengo yake katika kuzalisha wahitimu wenye ubora.
“Usafirishaji ni jambo linalohusisha wadau mbalimbali ambapo ili Taifa liweze kufikia katika uchumi wa juu kila mdau anapaswa kutekeleza ipasavyo jukumu lake, katika hili nachukua fursa hii kukipongeza chuo cha NIT kwa hatua hii inayoliwezesha Taifa kupiga hatua” amesema Bw.Johari.
Kwa upande wake Mkuu wa Chuo cha Usafirishaji Prof. Zacharia Mganilwa amesema ushirikiano na taasisi hizo umekuja wakati muafaka ambao NIT inatekeleza miradi ya uboreshaji wa elimu (ESTRIP) unaofadhiliwa na Benki ya Dunia.
Amesema kupitia ushirikiano na Chuo hicho itaweza kupiga hatua kwa kutatua changamoto mbalimbali za kiutendaji na taasisi hizo anaamini kutakiwezesha chuo hicho kutimiza malengo yake ya kuzalisha wataalamu wenye umahiri hususani katika sekta ya usafirishaji.
Naye Mkurugenzi wa kituo cha LHRC Bi.Anna Henga amesema anaamini kupitia ushirikiano huo watakiwezesha Chuo hicho kuongeza ufanisi wake sanjari na kuwa na uwiano sawa wa jinsia kwa wanafunzi na watumishi chuoni hapo.