Mkuu wa Wilaya ya Tabora Dkt. Yahya Nawanda akitoa nasaha zake jana katika Mahafali ya saba ya Chuo cha Tabora Polytechnic ambapo wahitimu zaidi 273 walitunikiwa stashahada katika fani za wafanasia, , elimu na malezi ya watoto, uandishi wa habari na utangaaji, utunzaji kumbukumbu, Uongozaji watalii na ukarimu na ukatibu Muhtasi .
Mkurugenzi wa Chuo cha Tabora Polytechnic Shabani Mrutu akitoa maneno ya utanguzi jana wakati wa Mahafali ya saba ambapo wahitimu zaidi 273 walitunikiwa stashahada katika fani za wafanasia, , elimu na malezi ya watoto, uandishi wa habari na utangaaji, utunzaji kumbukumbu, Uongozaji watalii na ukarimu na ukatibu Muhtasi .
Mwenyekiti wa Bodi ya Chuo cha Tabora Polytechnic Lucas Ndanga akitoa hotuba jana wakati wa Mahafali ya saba ambapo wahitimu zaidi 273 walitunikiwa stashahada katika fani za wafanasia, , elimu na malezi ya watoto, uandishi wa habari na utangaaji, utunzaji kumbukumbu, Uongozaji watalii na ukarimu na ukatibu Muhtasi .
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Dkt. Yahya Nawanda (kulia) akibadilisha mawazo jana na Mkurugenzi wa Chuo cha Tabora Polytechnic Shabani Mrutu(kushoto) wakati wa Mahafali ya saba ambapo wahitimu zaidi 273 walitunikiwa stashahada katika fani za wafanasia, , elimu na malezi ya watoto, uandishi wa habari na utangaaji, utunzaji kumbukumbu, Uongozaji watalii na ukarimu na ukatibu Muhtasi .akitoa nasaha zake jana katika Mahafali ya saba
Mkuu wa Wilaya ya Tabora Dkt. Yahya Nawanda (kushoto) akibadilisha mawazo jana na Mjumbe wa Bodi ya Chuo cha Tabora Polytechnic Dkt Mrisho Sango (kulia) wakati wa Mahafali ya saba ambapo wahitimu zaidi 273 walitunikiwa stashahada katika fani za wafanasia, , elimu na malezi ya watoto, uandishi wa habari na utangaaji, utunzaji kumbukumbu, Uongozaji watalii na ukarimu na ukatibu Muhtasi .akitoa nasaha zake jana katika
NA TIGANYA VINCENT
MKUU wa Wilaya ya Tabora Dkt. Yahya Nawanda amewataka Wazazi kuhakikisha wanawalea watoto wao katika misingi bora ili wasijihusishe na vitendo vya uhalifu ikiwemo wizi na ubakaji.
Alisema hali hiyo itawafanya kuwa na maadii bora na kuwasababishia kujihusisha na shughuli halali za kuwaingizia kipato.
Dkt.Nawanda alitoa kauli hiyo jana wakati wa Mahafali ya saba ya Chuo cha Tabora Polytechnic ambapo wahitimu zaidi 273 walitunikiwa stashahada katika fani za wafanasia, , elimu na malezi ya watoto, uandishi wa habari na utangaaji, utunzaji kumbukumbu, Uongozaji watalii na ukarimu na ukatibu Muhtasi .
“Niwaombe wazazi hao vibaka ni watoto wetu tuendelee kuwakanya na kuwalea katika misingi sahihi…mwisho siku mwisho wa mwizi ni mbaya… na kama umkanyi mtoto wako jamii itakmya itachukua nafasi ambayoutakuja kujitia” alisisitiza.
Aliwataka wazazi kuwaonya watoto wao kuachana na vitendo vya uhalifu vinginevyo watakutana na mkono wa sheria ikiwemo kufikishwa Mahakamani.
Dkt. Nawanda alisema Serikali ipo kwa ajili ya kulinda raia na mali zao na kama watashindwa kutii malezi ya wazazi wao watakuwa wamejiingiza kwenye mkono wa sheria.
Aidha aliwataka wazazi kuendelea katika uwekezaji katika elimu ya watoto wao ili hatimaye waweze kuwa wananchi wazuri ambao watashiriki katika ujenzi wa Taifa.
Dkt. Nawanda alisema uwekezaji wa elimu kwa watoto wao utasaidia kuwaondoa katika uhalifu na kufikiria zaidi katika shuighuli halali za maendeleo.
Alisema wataimarisha doria za usiku katika maeneo yote na Wilaya ya Tabora na kutengeza Polisi Jamii kwa lengo la kuwahakikishia wakazi wa Wilaya hiyo usalama wao na mali zao.
Dkt. Nawanda alisema tatizo la uhalifu litakomesha ili wananchi waweze kufanya shughuli zao halali bila hofu yoyote.
Alisema changamoto nyingine inayokikabili chuo hicho ubovu wa kipande cha barabara kutoka barabara kuu kuelekea Chuoni.