*****************************
Mbunge wa Jimbo la Bumbuli January Makamba ameahidi Kuendelea kulipigania na kulipeleka Bungeni suala zima la Changamoto ya barabara lilopo maeneo ya vijijini ili kuwepo usawa Kati ya mjini na vijijini.
Hayo ameyasema jana wakati akizungumza na wananchi wa kata ya Mponde kuhusu Serikali ya awamu ya sita ilivowapatia sh. 1.5 9 bilion kwaajili ya kujenga Barabara kwa kiwango cha lami na changarawe kwenye baadhi ya Barabara zilizopo kwenye Jimbo hilo.
Makamba alitaja barabara zitakazonufaika na fedha hizo kwa kujengwa kwa kiwango cha changarawe kuwa ni Barabara ya Mgwashi – Mbelei yenye urefu wa kilometa 23.8 ,Bumbuli -Mayo, Vulii- Mahezangulu hadi Magoma kilometa 15.4,Vuga – Mponde hadi Wena kilometa 21.2 na Balangai – Tamota na Vuliii yenye urefu wa kilometa 13.4,Soni -Mponde kilometa 13.4 pamoja na Bumbuli center itakayojengwa kwa kiwango cha lami.
Mbunge huyo alisema sio sawa kuona mjini wanajengewa barabara za juu na zinapanuliwa kila kukicha lakini vijiji ambako wapiga kura wengi wapo wanapata shida kupitisha mazao yao kutokana na barabara kuwa changamoto hasa wakati wa msimu wa mvua.
” Inauma mtu analima chai yake anapalilia mwenyewe lakini anashindwa kupeleka kiwandani sababu barabara inautelezi hii sio sawa kabisa” Aliongea Makamba
“Mimi huwa nawaambia wenzangu kama kweli tunaweka barabara za magorofa hatushindwi kuwasaidia watu wa vijijini kwani wanachotaka barabara zao zipitike wakati wote hasa kipindi cha mvua” Alisema Makamba
Alisisitiza kuwa lazima kuwepo na haki sawa katika kupeleka maendeleo ya nchi haiwezekani kwa Dar es Salamu tu kuna barabara moja ina njia nne mpaka sita ambapo alitolea mfano yaani barabara moja ni kama kiwanja cha mpira yaani barabara inakuwa kwenye kona ile na kona nyingine.
Aidha alieleza kuwa moja ya malengo makubwa ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Hassan Sulluhu ni kupambana na barabara za vijijini.
Aliongeza kwamba serikali imepanga ifikapo mwaka 2025 Watanzania wanaokipigia chama cha Mapinduzi kila mwaka angalau barabara zao ziwe zinapitika wakati wote sababu hao tunaowajengea za magorofa yawezekana baadhi yao hawapigi ata kura wakati wa uchaguzi.
Hata hivyo alisema yeye kama Mbunge kiu yake ni kuona wananchi wake wanaondokana na changamoto hiyo ambayo ni kero kubwa ukilinganisha na jiografia ya maeneo ya Jimbo la Bumbuli
Makamba ameanza rasmi ziara ya kukagua miradi ya maendeleo na kuweka mawe ya msingi katika Jimbo lake..