Home Mchanganyiko SERIKALI ITAHAKIKISHA ZAO LA MKONGE LINAIMARIKA-RC MALIMA

SERIKALI ITAHAKIKISHA ZAO LA MKONGE LINAIMARIKA-RC MALIMA

0

p> 

 Mkuu wa Mkoa
wa Tanga Adam Malima akizungumza wakati wa ziara yake ya kukagua ukarabati wa Mashine za
kuchakata mkonge ambapo awali zilikua chakavu hali iliyokua ikisababisha
kushuka kwa uzalishaji wa zao la Mkonge.

Mwenyekiti wa Bodi
ya Wadhamini kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Balozi Alli Siwa akizungumza
Afisa Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya Sisalana Elizaberth Kalambo akielezea jambo

Sehemu ya wananchi wakimsikiliza kwa umakini Mkuu wa Mkoa wa Tanga Adam Malima

NA OSCAR ASSENGA, KOROGWE

SERIKALI Mkoani Tanga imesema
itahakikisha zao la Mkonge linaimarika kutokana na ongezeko la mahitaji ya
bidhaa zitokanazo na zao hilo duniani yanayolenga kuachana na matumizi ya
bidhaa za Plastiki ambazo zina athari kwa Jamii. 

Kauli hiyo imetolewa na Mkuu wa Mkoa
wa Tanga Adam Malima wakati wa ziara yake ya kukagua ukarabati wa Mashine za
kuchakata mkonge ambapo awali zilikua chakavu hali iliyokua ikisababisha
kushuka kwa uzalishaji wa zao la Mkonge. 

Mkuu huyo wa mkoa alisema kwa miaka
mingi nguzo ya uchumi ya Mkoa huo ilikuwa zao la Katani na miaka 50 iliyopita
Tanga ilikuwa inazalisha tani 150,000 lakini baada ya marekebisho na nguvu
kubwa mkoa wa Tanga inazalisha tani 35000.

Alisema hivi sasa Serikali ya
Tanzania chini ya Rais Samia Suluhu imeweka mkakati wa makusudi wa kuzalisha
zao la Mkonge Kitaifa kutoka Tani 35,000 hadi kufikia Tani 120,000.

Aidha alisema mkakati huo unasimamiwa
na Waziri Mkuu Kasim Majaliwa ambao wakuu wa mikoa na wadau wengine wote
wamekuwa ni sehemu ya mpango huo mafanikio yake yapo hapa wilayani Korogwe.

Alisema ili kufikia Tani 100,000 za
Mkonge wanaweza kufikia huko kwa kushirikiana na wawekezaji wakubwa wakiwemo
Mohamed Interprises Limited, Amboni Platation,
Kwale, Palet.

Mkuu huyo wa mkoa aliekeza lakini
bodi inajua na ina maelekezo ya Waziri Mkuu na Serikali juu ya mkakati huo
maana yake wanataka kuwa na uzalishaji wa mkonge mkulima ashiriki kama mmiliki
wa uzalishaji huo na sio kama manamba na namna ya kufanya hivyo ni kupitia kwa
vyama vya ushirika Amcos kama serikali, Mrajis wa vyama wataanza kuwa na uwezo
wa uongozi na rasimali ili iweze kuwa na uzalishaji mkubwa zaidi.

Alisema vyama vya Ushirika (AMCOS) wana
ubia katika uzalishaji na Kampuni ya Sisalana ambayo inamilikiwa na Shirika la
Hifadhi za Jamii (NSSF) hivyo Sisisala lazima ijengewe uwezo wa kupokea  zao linalotoka kwa Mkulima kutokana na kwamba
hivi sasa Sisalana wanapokea Tani 6000 kwenye Amcos zote na wana uwezo wa
kupokea tani 11000 .

Aliseam hivyo yeye amefika na timu
yake kuweza kutengeneza mkakati ili hizo tani 11000 ziwafikie Sisalana na
zipate kuchakatwa na mkulima aweze kupata haki yake pamoja licha ya kwamba huko
kuna changamoto za pande zote mbili za Amcos na Sisalana na nyengine ambazo
lazima utatuzi wake upatikana kwa Serikali ikiwemo suala la miundombinu
inayopitisha

Awali akizungumza Mwenyekiti wa Bodi
ya Wadhamini kutoka Mfuko wa Taifa wa Hifadhi za Jamii (NSSF) Balozi Alli Siwa
alisema sheria ya kuanzishwa kwa mfuko huo inawaruhusu kuingia kwenye uwekezaji
ndio maana wameshiriki kwenye ziara ya Mkuu wa Mkoa kwenye Corona ambazo
zinamilikiwa na Kampuni ya SISALANA ambayo ni kampuni tanzu ya NSSF.

Alisema kampuni hiyo imepewa dhamana
ya kuendesha Corona tano kwa madhumuni ya kuweza kurejesha fedha za wanachama ambapo
wanaendesha shughuli za biashara hiyo kwa kushirikiana na Amcos kazi yao kubwa
ni kuchakata majani ya katani ili Amcos ziweze kuuza brashi ambayo inaitwa
Singa na wao wanaweza kupata tozo kwa ajili ya kuchakata.

Alisema hilo limewapelekea kwenye
biashara ya mkonge na kwao hiyo haitoshi kuchakata kutokana na kwamba
itawachelewesha kurudisha fedha zao wanazotaka kuzipata na pili wanataka
biashara hiyo iwe na maana katika kutunishia mfuko wa Pensheni ili waweze kuwa
na uwezo mkubwa wa kulipa pensheni kila inapohitajika kwa wanachama wao.

Naye kwa upande wake Afisa Mtendaji
Mkuu wa Kampuni ya Sisalana Elizaberth Kalambo alisema walianza kazi yao kwa
kufanya ukarabati katika mitambo katika kiwanda cha Usambara na baada ya hapo
watahamia Mwelya ili kuhakikisha mitambo inakuwa katika hali nzuri.

Alisema wakati wanafanya ukarabati
na matengenezo kwenye mitambo hivyo wanaomba wakulima wa mkonge wanaosimamiwa
na Amcos tano za Mwelya, Magoma, Hale, Ngombezi na Magunga wanaomba wakulima wawape
ushirikiano ili waweze kufanya maboresho.

Alisema kwa sababu wanapofanya
matengenezo makubwa wanasimamisha uzalishaji kwa muda wa usipoungua wiki mbili
mpaka tatau hivyo wanasisitiza kwa wakulima waongeze kasi ya upelekaji wa
majani kwa kupeleka awamu mbili ili kuepuka hasara watakazokutana nazo wakati
wanaposimamisha uzalishaji kwa siku hizo.