Home Biashara MSHINDI WA KAMPENI YA “TWENDE MJINI NA MPESA” AKABIDHIWA GARI AINA YA...

MSHINDI WA KAMPENI YA “TWENDE MJINI NA MPESA” AKABIDHIWA GARI AINA YA TOYOTA CRUISER

0

Mshindi wa gari aina ya Toyota cruiser mpya 2021 kwenye kampeni ya “TWENDE MJINI NA MPESA” Bi.Neema Ikolo akionesha plate number ya gari hilo leo katika hafla  ya kukabidhiwa zawadi kwa washindi wa kampeni ya “TWENDE MJINI NA MPESA” iliyofanyika leo Mlimani City Jijini Dar es salaam. 

Mkuu wa Kanda ya Dar es salaam na Pwani wa Kampuni ya Vodacom BrigIta stephen akimkabidhi ufunguo wa pikipiki mmoja wa washindi kutoka Temeke katika kampeni ya “Twende mjini na Mpesa ” ambapo zawadi hizo zimekabidhiwa kwa washindi leo Mlimani City Jijjini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kanda ya Dar es salaam na Pwani wa Kampuni ya Vodacom BrigIta stephen akimkabidhi ufunguo wa pikipiki mmoja wa washindi kutoka Kariakoo katika kampeni ya “Twende mjini na Mpesa ” ambapo zawadi hizo zimekabidhiwa kwa washindi leo Mlimani City Jijjini Dar es Salaam.

Washindi wa Kampeni ya “TWENDE MJINI NA MPESA” walioshinda pikipiki wakionesha funguo zao mara baada ya kukabidhiwa zawadi zao leo kwenye hafla ya kukabidhiwa washindi hao iliyofanyika leo Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Kanda ya Dar es salaam na Pwani wa Kampuni ya Vodacom Brigita stephen akizungumza katika hafla ya kuwakabidhi zawadi washindi wa Kampeni ya “TWENDE MJINI NA MPESA” iliyofanyika  leo Mlimani City Jijini Dar es Salaam. 

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wahuduma ya M-pesa Bi.Nelusigwe Mwangota akizungumza katika hafla ya kuwakabidhi zawadi washindi wa Kampeni ya “TWENDE MJINI NA MPESA” iliyofanyika  leo Mlimani City Jijini Dar es Salaam. 

Wacheza Dance wakitumbuiza kwenye hafla ya kuwakabidhi zawadi washindi wa Kampeni ya “TWENDE MJINI NA MPESA” iliyofanyika  leo Mlimani City Jijini Dar es Salaam. 

(PICHA ZOTE NA EMMANUEL MBATILO)

**************************

NA EMMANUEL MBATILO, DAR ES SALAAM

Kampuni ya Vodacom yakamilisha Kampeni yake ya “TWENDE MJINI NA MPESA”kwa kuwakabidhi zawadi zao washindi ambapo msindi mmoja amekabidhiwa gari aina ya Toyota cruise, mwingine kukabidhiwa bajaji na washindi wengeine watano wamekabidhiwa pikipiki.

Akizungumza na Waandishi Wahabari Mara baada ya kukabidhi zawadi kwa washindi hao Mkuu wa Kanda ya Dar es salaam na Pwani wa Kampuni ya Vodacom Brigita stephen amesema tulitoa bajaji moja kila wiki kwa wiki 8 na Leo inatoka gari aina ya Toyota cruise.

“Unapokua na M-pesa inarahisisha Maisha kutokana na kulipia nahitaji mbalimbali luku,umeme kununua bando na vingine vingi hivyo utaona mtandao wetu ilivokua na faida na Leo tumekabidhi pikipiki 5 kwa washindi ,bajaj moja pamoja na gari aina ya Toyota cruise “. Amesema Bi.Brigita 

Bi.Brigita ametoa rai kwa watumiaji ya wa Vodacom kuendelea kutumia mtandao huo vizuri ili waweze kufaidika na zawadi mbalimbali zinazotolewa na Vodacom.

Hata hivyo amewataka waliopokea zawadi hizo kuwa mfano mzuri na kuutangaza vizuri mtandao huo.

Nae Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wahuduma ya M-pesa Bi.Nelusigwe Mwangota ameeleza jinsi gani kampeni hiyo ilikua na lengo la kuwashika mkono wa Tanzania na Kuishi maisha ya kidigitali kutokana na kutumia Mpesa na kuwawezesha kufanya miamala kwa urahisi na kulipia bili mbalimbali.

“Tumeendelea kuwa wabunifu ambapo tumekua tukitatua matatizo mbalimbali tumebuni M_pawa,M_koba,songesha huduma zote hizi ni kwa ajili ya kuwezesha kupata mkopo kwa haraka.” amesema Bi.Nelusigwe.

Amesema wanawake wamekuwa wakiachwa nyuma lakini katika kampeni hii haajaachwa mtu wamekuwa pamoja na ndio maana Mshindi wa gari kwemye kampeni hiyo ni Mwanamke.

“Promosheni ambayo imechukua jumla ya week 8 katika Mikoa mbalimbali na Leo imefika tamati kwa kuwakabidhi zawadi za washindi wa Mkoa wa Dar es salaam na Pwani”. Ameongeza Bi.Nelusigwe.

Kwa upande wake aliyeibuka Mshindi wa gari aina ya Toyota cruiser mpya 2021 Bi.Neema Ikolo ameipongeza Kampuni hiyo kwa kuendesha kampeni hiyo ya Twende Mjini na Mpesa ambayo imetimiza ndoto za watu wengi ikiwemo yeye binafsi.

“Mara ya kwanza napigiwa simu sikuamini kabisa nilijua ni matapeli lakini baadae ni kapokea simu nikamsikia salama jabir aliongea ndipo nilipoamini nashukuru Sana Vodacom kwa kampeni hiyo itakayoenda kubadilisha maisha ya wengi Sana hususani watu wenye Hali ya chini”. Amesema Bi.Neema.

Bi.Neema ameeleza Sababu ambayo anahisi imemfanya kuibuka Mshindi wa gari katika kampeni hiyo ni pamoja na manunuzi ya vitu kwa kwa kutumia M-pesa ndio sababu iliyochangia kushindaShindano hilo.