Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akikologa udongo kwa ajili ya kukamilisha darasa linalojengwa kwa fedha za mradi wa EP4R katika Shule ya Sekondari Bulungwa iliyoko Halmashauri ya Ushetu jana Mkoani Shinyanga.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akikagua ujenzi wa madarasa mawili yanayojengwa katika shule ya Msingi Bugomba B kwa lengo la kukabiliana na msongamono katika shule hiyo.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati akiongea na wanafunzi wa Shule ya Sekondari Burungwa alipofika hapo jana kujionea ujenzi wa vyumba vya madarasa shuleni hapo jana.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Senganti akisalimiana na wanafunzi wa darasa la pili wa Shule ya Msingi Bugomba A jana alipofika shuleni hapo kwa lengo la kujionea miradi ya ujenzi inayotekelezwa kwa miradi ya EP4R.
………………………………………………………………
Na Anthony Ishengoma-Shinyanga
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Dkt. Philemon Sengati ametaka kuharakisha kwa ujenzi wa vyumba vya madarasa kwa shule za msingi tatu zenye takribani wanafunzi 2,000 kila moja zilizoko kata ya Ulewe Halmashauri ya Ushetu nakutaka ujenzi huo kamilika ifikapo Agosti 30.
Shule hizo ambazo ni Nyalwelwe, Bugomba A na B zina msongano mkubwa wa wanafunzi uku vyumba vya madarasa katika shule izo vikiwa ni vichache na kusababisha baadhi ya wanafunzi kupata huduma ya masomo katika mabanda ya muda yaliyotayalishwa na uongozi wa shule kwa kushirikiana na wazazi.
Dkt. Philemon Sengati alijionea hali hiyo baada ya kufika katika Shule izo kujionea maendeleo ya ujenzi ya mradi wa ujenzi wa vyumba vya madarasa vinavyojengwa kwa msaada wa mradi wa EP4R inayoendelea katika Halmashauri zote za Mkoa wa Shinyanga.
‘’Hali ndiyo hii hairidhishi, sasa mnakwama wapi mnatakiwa mpate suluhisho haraka muongeze kasi ya ujenzi vinginevyo naweza kuchukua maamuzi mengine mabaya dhidi yenu kwasababu hatufurahishwi na hii hali ambayo haitamfurahisha mtu yeyeyote atakayeiona kwahiyo hatuitaki hii hali’’. Alinukuliwa akisema Dkt. Sengati Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga.’’
Dkt. Sengati aliongeza kuwa mazingira ya wanafunzi ambayo wanasomea kwasasa sio mazuri kutokana na kuwapo kwa msongamano mkubwa madarasani na hivyo kuwataka kuwa wabunifu zaidi kwa kuwa wanatumia tofali za kuchoma jambo ambalo litawawezesha kuongeza vyumba zaidi kutokana na kuokoa kiasi cha pesa ambacho ukichanganya na nguvu za wananchi wanaweza kupunguza kwa kiasi kikubwa msongamano huo.
Naye diwani wa kata ya Ulewe Bw. Kulwa Mabula alisema Shule izo zinakabiliwa na Msongano mkubwa wa wanafunzi kutokana na watu wengi wanaohamia katika kata hiyo ambayo inarutuba sana na wanahamia hapo kwa ajili ya shughuli za kilimo kutoka sehemu mbalimbali jilani na Wilaya ya Kahama na eneo hilo ni fursa kwa biashara mbalimbali.
Mkuu wa Shule Burungwa Bw. Richard Mgana alikili kuwepo kwa changamoto kubwa ya msongamano mkubwa inayoathiri ufundishaji na kujifunza kwa kuwa ni vigumu kwa walimu kufanya ufuatiliaji kwa mwanafunzi mmoja mmoja.
Bw. Mgana aliongeza kuwa pamoja na changamoto hiyo aliiomba serikali pia kujenga shule mpya katika Kata hiyo kwa kuwa eneo hilo kwa sasa lina idadi kubwa ya watu na suluhisho la kudumu litakuwa ni kuanzishwa kwa shule mpya.
Afisa Elimu Mkoa wa Shinyanga Bi. Dafroza Ndalichako akitoa sababu za kuchelewa kwa fedha za ujenzi wa vyumba vya madarasa katika baadhi ya Shule za Halmashauri hiyo alisema linachangiwa taratibu za kimfumo lakini pia akaangazia uwezo mdogo wa kifedha wa mafundi wa sehemu za vijijini ukilinganisha na wale wa Manispaa kama vile Kahama.
Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga anaendelea na ziara yake katika Wilaya za Mkoa wa Shinyanga na tayari amefanya ziara kama hiyo katika Wilaya ya Kishapu, Manispaa ya Kahama na ataendelea na ziara kama hiyo katika Halmashauri ya Msalala kukagua miradi ya maendeleo ya ujenzi wa vyumba vya madarasa ikiwemo miradi inayotekelezwa kwa fedha za miradi ya EP4R.