Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Zainab Chaula,wakati akifungua Kikao cha Wizara na Taasisi zake kuhusu ukaguzi wa ndani cha uandaaji wa vitabu vya hesabu na utekelezaji wa mapendekezo ya ripoti ya CAG kilichofanyika leo Julai 29,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Zainab Chaula,akifafanua jambo kwa washiriki wakati wa Kikao cha Wizara na Taasisi zake kuhusu ukaguzi wa ndani cha uandaaji wa vitabu vya hesabu na utekelezaji wa mapendekezo ya ripoti ya CAG kilichofanyika leo Julai 29,2021 jijini Dodoma.
Mkaguzi wa Ndani Mkuu kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari CPA Joyce Christopher,akizungumza wakati wa Kikao cha Wizara na Taasisi zake kuhusu ukaguzi wa ndani cha uandaaji wa vitabu vya hesabu na utekelezaji wa mapendekezo ya ripoti ya CAG kilichofanyika leo Julai 29,2021 jijini Dodoma.
Baadhi ya washiriki wakimsikiliza Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Zainab Chaula,(hayupo pichani) wakati akifungua Kikao cha Wizara na Taasisi zake kuhusu ukaguzi wa ndani cha uandaaji wa vitabu vya hesabu na utekelezaji wa mapendekezo ya ripoti ya CAG kilichofanyika leo Julai 29,2021 jijini Dodoma.
Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Zainab Chaula,akizungumza na waandishi na habari mara baada ya kufungua Kikao cha Wizara na Taasisi zake kuhusu ukaguzi wa ndani cha uandaaji wa vitabu vya hesabu na utekelezaji wa mapendekezo ya ripoti ya CAG kilichofanyika leo Julai 29,2021 jijini Dodoma.
Mkaguzi wa Ndani Mkuu kutoka Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari CPA Joyce Christopher,akizungumza na waandishi na habari mara baada ya Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Zainab Chaula kufungua Kikao cha Wizara na Taasisi zake kuhusu ukaguzi wa ndani cha uandaaji wa vitabu vya hesabu na utekelezaji wa mapendekezo ya ripoti ya CAG kilichofanyika leo Julai 29,2021 jijini Dodoma.
Mkaguzi wa Ndani Mkuu kutoka Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL) Bw.Octavian Barnabas ,akizungumza na waandishi na habari mara baada ya Katibu Mkuu Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Dkt Zainab Chaula kufungua Kikao cha Wizara na Taasisi zake kuhusu ukaguzi wa ndani cha uandaaji wa vitabu vya hesabu na utekelezaji wa mapendekezo ya ripoti ya CAG kilichofanyika leo Julai 29,2021 jijini Dodoma.
………………………………………………………
Na Alex Sonna,Dodoma
TAASISI sita za Wizara ya Mawasilino na Teknolojia ya Habari zimekutana Jijini Dodoma lengo likiwa ni kujadili jinsi ya uandaaji wa vitabu vya Hesabu na utekelezaji wa mapendekezo ya ripoti ya Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).
Akifungua kikao kazi hicho,leo Julai 29,2021,Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasilino na Teknolojia ya Habari,Dkt.Zainabu Chaula amesema wameamua kwa pamoja wakae kupeana AB kwani mwaka jana walikuwa hawajafanya vizuri na kulikuwa na sintofahamu katika Taasisi mbili.
“Hichi kikao tulikipanga na ni cha mkakati kwa sababu masuala ya ukaguzi yapo kisheria katika Taasisi sita zinapaswa pia kufuata sheria hizo kazi ya kiongozi ni kuhakikisha kanuni,taratibu na sheria zinafuatwa binadamu bila kumfuata kwa karibu tegemea kufeli,”amesema.
“Katika Taasisi wapo waliofanya vizuri lakini wapo waliokuwa na Kwere za kutosha na kweli mara nyingi tunazitengeneza wenyewe kwahiyo wao kama wahasibu wa ndani ambao tumewapa jicho la kwanza haya ni maandalizi ili mkaguzi mkuu wa Serikali akija akute mambo yamekaa sawa sio kwa kutengeneza tunataka kutengeneza utamaduni huu,”amesema.
Amesema wameamua kuweka utaratibu huo kwa sababu mara nyingi wanapokuja wakaguzi wanakuta baadhi ya vitu havipo sawa hivyo wanatengeneza utamaduni wa uwajibikaji wa pamoja.
“Tunatengeza utamaduni wa uwajibikaji wa pamoja,kwa sababu mara nyingi wanapokuja wakaguzi wanakuta baadhi ya vitu havipo natamani kuna mambo mengine ni ya msingi lakini hatuyatekelezi sasa hapa nimekuja kuwaambia nini tunatarajia na wamekuja wahasibu na wakaguzi wa ndani wao ndio wanapaswa kuwasaidia,”amesema Katibu Mkuu.
Kwa upande wake Mkaguzi wa ndani Mkuu wa Wizara ya Mawasilino,Teknolojia ya Habari,CPA Joyce Christopher amesema wapo kwa ajili ya kikao kazi ambapo Taasisi sita zimejumuika wakiwemo wakaguzi wa ndani na wahasibu ambapo lengo ni kupanga mipango ya pamoja jinsi ya kufunga mwaka.
Amesema agenda ya pili ni utekelezaji wa hoja zilizoibuliwa na CAG na kuzifanyia kazi ili ziweze kufungwa mwaka 2020-2021 asikute hoja.
“Majukumu ya kitengo cha ndani katika kuhakikisha hoja za CAG zinafanyiwa kazi lengo ni kuboresha na kuhakikisha tunafanya vizuri pia kuangalia thamani ya fedha za Serikali zinaonekana,”amesema CPA Joyce.
Naye,Mkaguzi wa Ndani Mkuu kutoka Shirika la Mawasilino Tanzania (TTCL) Octavian Barnabas amesema lengo la kikao hicho ni kupunguza hoja zilizotokana na Ofisi ya CAG ambapo kwa pamoja wataibuka na majibu nini kifanyike ili kusiwe na kwere.