Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akizungumza na waandishi wa habari kuarifu umma kuhusu kikao cha mapato na matumizi kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha 2020/2021 cha Menejimenti ya Wizara na taasisi zake kilichofanyika Dodoma
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Zainab Chaula akiendesha kikao cha kuthamini mapato na matumizi cha robo ya nne ya mwaka wa fedha wa 2020/21 cha Menejimenti na taasisi za Wizara hiyo kilichofanyika Dodoma
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile akiteta jambo na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula wakati wa kikao cha kutathmini mapato na matumizi ya robo ya nne ya mwaka wa fedha wa 2020/21 cha Wizara hiyo na taasisi zake kilichofanyika Dodoma
Kaimu Mkurugenzi wa Sera na Mipango wa Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Joyce Momburi (wa kwanza kulia) akifuatilia uwasilishaji wa taarifa ya mapato na matumizi ya robo ya nne ya Wizara na taasisi zake kilichofanyika Dodoma
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote, Justina Mashiba (kulia) wakifuatilia wasilisho la taarifa ya mapato na matumizi ya robo ya nne ya mwaka wa fedha wa 2020/21 ya Wizara na taasisi zake kwenye kikao kilichofanyika Dodoma
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania, Dkt. Jabir Bakari akiwasilisha taarifa ya mapato na matumizi ya robo ya nne ya mwaka wa fedha wa 2020/21 ya taasisi yake kwenye kikao cha Menejimenti ya Wizara ya Mawasiliano na Teknolojia ya Habari na taasisi zake kilichofanyika Dodoma
…………………………………………………………………………
- Ajipanga Kuzima Laini za Simu Ambazo Hazijahakikiwa
- UCSAF, TTCL na TPC zaongeza makusanyo ya mapato
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Dkt. Faustine Ndugulile ameendesha kikao cha mapato na matumizi ya robo ya nne ya mwaka wa fedha wa 2020/21 baina ya menejimenti ya Wizara hiyo na taasisi za Wizara hiyo ikiwemo Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA), Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Shirika la Posta Tanzania (TPC), Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Tume ya TEHAMA (ICTC) na Baraza la Watumiaji wa Huduma ya Mawasiliano (TCRA – CCC) ambacho kimefanyika kwenye ukumbi wa Kikwete, Dodoma
Ameongeza kuwa kwa kipindi hicho cha mwezi Aprili hadi Juni, 2021, Wizara kwa kushirikiana na taasisi zake imefanikisha utekelezaji wa majukumu yake ya kuongeza mapato ya taasisi hizo ikiwemo taasisi ya UCSAF, TTCL na TPC.
Amesema kuwa ameazimia kuzima laini za simu za mkononi 18,622 ambazo hazijahakikiwa pamoja na kuziua vitambulisho vya taifa 14,768 vilivyosajili laini za simu kwa utapeli na Serikali itawatafuta matapeli hao ili waweze kuchukuliwa hatua
Katibu Mkuu wa Wizara hiyo, Dkt. Zainab Chaula amesema kuwa kikao hicho kimefanyika ili kufanya tathmini ya utekelezaji wa majukumu na mapato na matumizi ambapo Wizara imekusanya mapato ya Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano ya shilingi bilioni 45 ambayo yamezidi makadirio ya shilingi bilioni 30. Pia, ameishukuru Serikali kwa kuongeza bajeti ya Wizara ya mwaka wa fedha wa 2021/22 kufikia shilingi bilioni 240 ukilinganisha bajeti ya shilingi bilioni 15 ya mwaka wa fedha 2020/21.
Naye Kaimu PostaMasta Mkuu wa Shirika la Posta Tanzania (TPC), Macrice Mbodo amesema kuwa huu ni utaratibu mzuri baina ya Wizara na taasisi zake kwa kuwa kila baada ya miezi mitatu kikao kinafanyika na kwa kipindi hicho Shirika limezalisha faida ya shilingi bilioni 3.6; kuboresha huduma ya duka mtandao ambapo wajasiriamali wadogo wanafanya biashara duniani kote
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Mawasiliano Tanzania (TTCL), Mwita Vedastus amesema kuwa Shirika limepata faida ya shilingi bilioni 12 kwa mwaka na kwa robo ya nne ya mwaka wa fedha wa 2020/21 wamepata faida ya shilingi bilioni 2 kwa mapato ambayo hayajakaguliwa pamoja na kutoa huduma ya data kwa wateja 223,000 wa taasisi za ndani na nje ya nchi na watu binafsi
Afisa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF), Justina Mashiba amesema kuwa kikao hicho kinawezesha kupeana mrejesho baina ya Wizara na taasisi zake ili kufahamu mapato na matumizi kwa kipindi hicho ambapo UCSAF imezidi malengo kwa kukusanya mapato ya shilingi bilioni 9 tofauti na makadirio yaliyopangwa awali ya kukusanya shilingi bilioni 8
Ameongeza kuwa wamefanikisha ujenzi wa minara 60 ambayo imekamilika na kutangaza zabuni za kupeleka mawasiliano mipakani katika kata 190 na halmashauri 10 kwa kuwa zinahamia majengo mapya ili wapate huduma za mawasiliano