Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali wa Wizara ya Habari,Utamduni, Sanaa na Michezo ndugu Bernad Marcelline akizungumza na watumisha wa wizara hiyo
Watumishi wakimsikiliza Mkurugenzi huyo Adeladius Makwega
******************************
Mtumba- WHUSM
Watumishi wa umma wanapaswa kufahamu kuwa malalamiko yoyote yanayotolewa au kulalamikiwa Serikali ni ya watumishi wa umma, hivyo, kuyaondoa malalamiko hayo ni wajibu wa watumishi wote wa umma kufanya kazi kwa bidii.
Kauli hiyo ya serikali imetolewa leo na Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali Watu wa Wizara ya Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo Bw. Bernad Marcelline wakati akizungumza na watumishi wa Mkao Mkuu wizara hiyo zilizopo katika Mji wa Serikali Mtumba Jijini Dodoma katika mafunzo ya namna bora ya ujazaji wa Fomu ya Mfumo wa Wazi wa Mapitio na Thamini ya Utendaji kazi (OPRAS).
“Juhudi ya kazi Serikalini ni jambo la msingi na linapimwa na fomu ya OPRAS, kama itajazwa vizuri kutoka sehemu ya kwanza hadi ya nane, na ujazaji huo uambatane na hali halisi ya kufanyakazi kw ajuhudi na maarifa ya mtumishi husika” alisema.
Bw. Marcelline ameongeza kuwa pale yanapoibuka malalamiko ya kweli tambua kuwa kuna pahala mmoja wapo miongoni mwa watumishi hajatekeleza wajibu wake.
“Baadhi ya watumishi unaweza kumtafuta baada ya muda wa ziada kufanya kazi fulani hapatikani, jambo hili linakuwa kero, pengine kiongozi anahitaji ufafanuzi wa haraka kuhusu jambo fulani na simu inapopatikana jambo linakuwa tayari limeshakwama” aliogeza Mkurugenzi huyo wa Utawala na Serimali Watu.
“Ujazaji huo wa fomu za OPRAS unatakiwa kufanya kwa umakini kwani si jambo jema kuona kuwa mtumishi anapata wastani wa nne na tano na vile vile mtu kupata alama moja. Si dhambi lakini unaweza kufanya hivyo kama jambo hilo lina ushahidi wa kutosha” aliongeza Mkurugenzi Marcelline.
Mtumishi anayepata wastani wa nne na tano kwa mujibu wa taratibu za utumishi wa umma anapaswa kufukuzwa kazi ndiyo maana inapojazwa lazima pawepo na vielelezo vya kutosha kwa alama hizo.
Naye Mkurugenzi wa Sera na Mipango Petro Lyatuu akizungumza katika mafunzo hayo amesema kuwa ni wajibu wa pande zote mbili za mtumishi na msimamizi kuhakiksha fomu hiyo inajazwa vizuri kwani ni nyaraka muhimu ya Serikali.
“Fomu hii inaweza kutumiwa wakati wowote na ni lazima ijazwe kwa umakini ni siyo holela, inakaa kwenye fili la mtumishi hadi atakapostaafu.” Alisema Mkurugenzi huyo wa Sera na Mpango.
Wakizungumza katika mafunzo hayo baadhi ya watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wamesema kuwa mafunzo hayo yamekuwa na tija sana kwao na inasadia sana kila mtumishi kutambua wajibu wake na kujaza fomu hii kwa usahihi.
“Mafunzo haya yamenisadia sana, hapo baadaye itakuwa vizuri kama fomu hizo tukazijaza kwenye mtandao ili ziweza kupatikana kwa urahisi pale zinapohitajika” alisema Gervas Mbilinyi kutoka Idara na Sera na Mipango ya Wizara hiyo.
Mafunzo hayo yalianza Julai 27,2021 yanatarajiwa kukamilika Julai 30,2021 ambapo watumishi wa idara zote za Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na MIchezo wanashiriki.