Home Mchanganyiko CORONA IPO WATUMISHI WA UMMA ZINGATIENI MAELEKEZO YA WIZARA YA AFYA

CORONA IPO WATUMISHI WA UMMA ZINGATIENI MAELEKEZO YA WIZARA YA AFYA

0

Mtumishi wa Idra ya Sera na Mipango Davie Kabiga akinawa soma tnagzo la kuvaa  barako na pia kinawa mikono yake  katika Kipukusi

………………………………………………………………….

Adeladius Makwega,Mtumba- WHUSM

Watumishi wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo wametakiwa kufuata maelekezo ya Serikali juu ya Uviko 19 kwani ugonjwa huo ni hatari kwa maisha ya binadamu na unaua watu katika maeneo mbalimbali duniani.

Kauli hiyo imetolewa leo Julai 28, 2021 na Mkurugenzi wa Utawala na Rasimali Watu wa Wizara hiyo Bw. Bernad Marcelline wakati wa mafunzo yanayohusiana na ufanyaji kazi bora wa watumishi wa umma.

“Watu wanafariki kutokana na Korana hilo halina ubishi, ndiyo maana Serikali imekuwa inatoa maelekezo mengi ya namna ya uvaaji wa  barakoa na kunawa mikono kwa kutumia kipukusi ili kulinda  afya zetu” amesema Mkurugenzi  Marcelline katika mafunzo hayo.

Kunawa mikono kwa kipukusi na kuvaa barakoa kunasaidia kujilinda wewe mwenyewe, watumishi wenzako, familia yako nyumbani na kuwalinda Watanzania wengine aliongeza kiongozi huyo wa wizara hii.

“Unaweza kuona kuwa ugonjwa huu haupo kwa kuwa janga hilo halijakufika, lakini nakwambieni janga hili lipo na la msingi ni kufuata tu maelekezo yote ya kanuni za afya yanayotolewa na Wizara ya Afya, Maendeleo Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kila siku” ameongeza.

Wakizungumza mara baada ya mafunzo hayo watumishi wa wizara hiyo wamesema wameshaanza kutekeleza agizo hilo tangu lilipotolewa hapo awali na wanaihakikishia Serikali kuwa wataendelea kuelimisha umma kupitia vyombo vya habari juu ya ugonjwa huo.

“Sisi ni wizara ya inayoshughulikia habari na michezo tunawapasha habari Watanzania wote juu ya Korana na tunasisitiza watumishi na wananchi kwa ujumla tufanye mazoezi” alisema Daviez Kabigi ambaye ni mtumishi wa Idara ya Ununuzi na Ugavi wizarani hapo.

Kabigi ameongeza kuwa leo amemuona Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan akichanjwa na yeye amesema chanjo hiyo ikifika Dodoma atakuwa wa kwanza kufanya hivyo kutekeleza agizo la Serikali.

Wizarani hapo kwa sasa yamewekwa mazingira bora ya kupambana na Korana kwa kwa kuweka ndoo ya kunawia mikono kwa maji tiririka, kuwepo na sehemu  maalumu ya  kipukusi na huku kukiwa na matangazo ya tahadhari kwa watumishi na watu wengine wanaokuja  kupata huduma.