Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Taifa (UVCCM) Bw. Kenan Kihongosi,akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 27,2021 jijini mara baada ya kumalizika kwa kikao cha sekretarieti ya UVCCM.
Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Taifa (UVCCM) Bw. Kenan Kihongosi,akisisitiza jambo kwa waandishi wa habari leo Julai 27,2021 jijini mara baada ya kumalizika kwa kikao cha sekretarieti ya UVCCM.
……………………………………………………………………………
Na.Alex Sonna, Dodoma.
Katibu wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana Taifa (UVCCM) Bw.Kenan Kihongosi ametaka Chama cha Mapinduzi CCM taifa kuwachukulia hatua kali za kinidhamu viongozi wa serikali na chama wanaotoa kauli za kuwapotosha wananchi juu ya chanjo za ugonjwa wa Corona COVID 19.
Katibu huyo ameyabainisha hayo leo Julai 27,2021 jijini Dodoma wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumalizika kwa kikao cha sekretarieti ya UVCCM, ambapo amesema ambapo amesema wao wamesikitishwa na kitendo cha Mbunge wa Jimbo la Kawe Askofu Josephat Gwajima kupitia Chama cha Mapinduzi CCM kuwataka wananchi kukataa kuchajwa chanjo ya kuzuia virusi vya Corona.
“Sisi kama vijana wa umoja wa chama cha mapinduzi tunalaani vikali kitendo cha mbunge wa Jimbo la kawe kwa kutoa kauli kwa wananchi kuikataa chanjo kwamba wakichanjwa watakufa,”.
Nakuongeza kuwa ” Inasikitisha sana kuona kiongozi wa dini wanapotosha umma na kutoa matamko ya vitisho kwa wananchi ilihali anayetoa uhai ni Mungu na anae amua kutomchukua mja wake ni Mungu, Sisi Kama Vijana wa CCM tutasimama na Rais wetu kwakuwa tayari muongozo ulishatolewa chanjo ni hiari sio lazima”amesema Kihongosi
Aidha amewata viongozi wachama kuacha kutoa matamko holela bila kufuata taratibu za muongozo wa wizara ya Afya juu ya ugonjwa wa vurusi vya Corona COVID 19.
Hata hivyo amewatoa hofu wananchi kwamba chanjo hiyo ni salama na Rais wa awamu ya Sita Samia Suluhu Hassan atakuwa wakwanza kuzindua chanjo hiyo .
Katika hatua nyingine amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa hatua anazochukua za kuchochea maendeleo ya nchi na wao kama vijana watamuunga mkono kwa kufanya kazi kwa bidii.