Meneja mauzo Kanda ya kaskazini kutoka kampuni ya TFA ,Renati Kauki ( mwenye tisheti nyeupe) akizungumza na mmoja wa wakulima kuhusiana na shughuli wanazofanya alipotembelea katika banda lao kwenye maonesho ya 8 ya kilimo biashara yaliyofanyika mjini hapa (Happy Lazaro).
**************************
Happy Lazaro, Arusha
Arusha.Kampuni ya usambazaji wa pembejeo za kilimo Tanzania (TFA) imeleta suluhisho kwa wakulima kwa kuja na pembejeo mpya ya kurutubisha udongo ijulikanayo kama TFA Fahari .
Akizungumzia kuhusiana na pembejeo hiyo .
,Meneja mauzo Kanda ya kaskazini ,Renati Kauki amesema kuwa,wamefikia hatua ya kuja na pembejeo mpya kwa lengo la kuwasaidia wakulima kuweza kuboresha kilimo chao kwa kuwa na udongo wenye rutuba vizazi na vizazi.
Kauki amesema kuwa, pembejeo hiyo ambayo ni kirutubisho udongo kinasaidia kurutubisha udongo na kuwezesha kupatikana kwa mazao mengi na yenye rutuba kwani pembejeo hiyo inafanya udogo uendelee kuwa bora zaidi.
“Tunawasihi wakulima wetu popote walipo kutumia pembejeo hii ambayo ni mpya kwani inaboresha afya ya udongo na kumsaidia mkulima kuzalisha zaidi kwani inaongeza mavuno mara dufu ,Kama mkulima alikuwa anavuna gunia mbili pembejeo hii inafanya uvune magunia manne na zaidi kwani imefanyiwa utafiti na ina faida nyingi Sana kwa wakulima.”amesema Kauki.
Ameongeza kuwa, pembejeo hiyo ni aina ya virutubisho maalumu kwa ajili ya udongo utakaotumika kwa kilimo cha aina yoyote ,kwani haina chumvi chumvi kama zilivyo mbolea nyingine,imetokana na mabaki ya mimea maalumu inayotumika kutengeneza maarufu kama.(sugar Beet).
Amefanua kuwa, kirutubisho hicho ni mahususi kutoka nchini Ufaransa ndani ya bara la Ulaya ambapo ina manufaa makubwa Sana katika kilimo kwani inatumika kupandia ,kukuzia mimea ikiwa na muda wa wiki 2 hadi 3.
Kauki amesema kuwa, endapo wakulima watatumia mbolea hiyo inaboresha afya ya udongo na kuondoa umaskini wa virutubisho kwenye udongo vinavyohitajika na mimea ili kuongeza mavuno.
Hata hivyo amewataka wakulima hao kutumia pembejeo hiyo kwani inasaidia kusawazisha tindikali magadi na tindikali chumvi na hivyo kuwezesha mimea kustawi vizuri ikiwa ni pamoja na kuzuia udongo kupoteza unyevunyevu kwa haraka huku ikilinda mazingira kwa vizazi vya sasa na vijavyo,kwani inalenga kutunza mazingira.
Kauki ameongeza kuwa, pembejeo hiyo inachangamana na mbolea nyingine kwa urahisi na kuongeza ufanisi wa matumizi ya mbolea kwa faida kubwa zaidi,hivyo kupunguza gharama kubwa ya mbolea .
Amesema kuwa,TFA ina matawi 17 nchi nzima na kuwa wamekuwa wakizunguka katika mikoa mbalimbali kwa lengo la kusikiliza changamoto za wakulima huku wengi wao wakilalamikia matumizi ya mbolea wanazotumia kutoleta matokeo mazuri ,hivyo kupitia pembejeo hiyo wakulima wataweza kuondokana na changamoto hiyo na kuweza kulima kilimo chenye tija .