*RC: Wekezeni katika miradi rafiki
*Msikurupuke kuanzisha miradi, jifunzeni kwanza
*Aipongeza PSSSF kwa semina
Na Mwandishi Wetu,
Mwanza
MKUU wa Mkoa wa Mwanza, Mhe.
Mhandisi Robert Gabriel amewashauri Wastaafu watarajiwa wa Mfuko wa Hifadhi ya
Jamii kwa Watumishi wa Umma (PSSSF) kuwekeza katika miradi waliyoizoea ili
waweze kuindesha vyema na kwa faida.
Mhandisi Gabriel alisema hayo
Jijini Mwanza wakati wa ufunguzi wa Semina ya Wastaafu watarajiwa kwa wanachama
wa PSSSF wa mkoa wa mwanza inayofanyika Julai 26 hadi 27, 2021.
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza
Mhe. Mhandisi Robert Gabriel, akihutubia wakati akifungua semina ya Wastaafu
watarajiwa wa PSSSF. Kulia ni Mwakilishi wa Mkurugenzi wa PSSSF, Bi. Beatrice
Musa-Lupi na katika ni Bi. Nyamisinda Manyunyi kutoka NMB.
“Kama unataka kuingia katika mradi
wowote, hakikisha unaonana na wataalamu ili waweze kukusaida katika
uwekeza sahihi na wenye tija,” alisauri Bw. Gabriel
Aliwashauri wastaafu hao watarajiwa
watakapolipwa mafao yao wasikurupuke kuanzisha miradi bali yajifunze vyema
mradi wanaotaka kuwekeza ili wajue njia sahihi ya kuwekeza katika mradi huo
“PSSSF wameletea Mabenki na Taasisi
mbalimbali ili muweze kupata uelewa na maarif ili mfanye maamuzi sahihi ya
uwekezaji. Hivyo tumieni fursa vyema, hii bahati kubwa kwenu, kwani sio wote
wanaopata fursa kama hii,” alisema Mkuu wa mkoa wa Mwanza.