**************************
NA VICTOR MASANGU.MAGINDU.
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani (CCM) Hawa Mchafu katika kuhakikisha anatekeleza ilani ya Chama ameamua kuchangia matofali Mia 500 kwa ajili ya ujenzivwa ofisi ya CCM kata ya kibindu iliyopo halmashauri ya kibaha vijiji.
Mchafu amekabidhi matofali hayo kwa uongozi wa Chama ngazi ya kata kwa ajili ya kuanza ujenzi huo ambao utasaidia kwa kiasi kikubwa viongozi wa CCM kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
Katika ziara hiyo Mchafu aliongozana na viongozi mbali mbali wa Chama ngazi ya Wilaya pamoja na wajumbe wa kamati ya siasa ya UWT katika halmashauri ya kibaha vijiji kwa lengo ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo.
Pia alisema ameamua kufanya ziara yake ya kikazi kwa kutembelea katika maeneo mbali mbali ikiwemo mkuranga.kibiti.kibaha mji pamoja na kibaha vijijini pamoja na kutoa msaada wa mifumo ya saruji pamoja ya michanga ili kusaidia sekta ya elimu,afya,pamoja na kusaidia wanawake wajasiriamali na vikundi.
Pia alisema kuwa lengo la serikali ya awamu ya sita ni kuhakikisha kwamba inawasaidia wananchi kuweza kuwapa sapoti ya kuwawezesha kiuchumi ili waweze kuondokana na wimbi la umasikini.
Akiwa katika ziara yake katika halmashauri ya kibaha vijijini pia aliweza kupata fursa ya kutembelea kikundi cha kufyatua matofali kilichopo kata ya mtongani na kutoa msaada wa mifumo 25 ya sarufi.
“Ndugu zangu nipo katika ziara yangu ya kikazi katika mkoa wa Pwani na lengo langu kubwa ni kupita katika baadhi ya Wilaya kugagua miradi ya maendeleo sambamba na kuchangia mifuko ya saruji katika kusaidia maendeleo katika nyanja tofauti;”alisema Mchafu.
Kadhalika aliwaomba wanachama wa Chama Cha mapinduzi hususan wanawake wa UWT kuendeleza ushirikiano naye kwa nia ya kuleta mapinduzi katika suala zima la maendeleo kwa wananchi wa Mkoa wa Pwani.
Katika hatua nyingine alikutana na viongozi mbali mbali wa CCM kata ya magindu ili kusikilizwa kero na changamoto zinazowakumba ili kuzitafutia ufumbuzi.
Baadhi ya viongozi wa CCM kata hiyo ya magindu walimueleza Mbunge huyo kuwa Kuna changamoto katika baadhi ya maeneo ikiwemo suala la ukosefu wa maji Safi na salama pamoja na ukosefu wa madaktari katika zahanati yao ya kibindu.
Akijibu hoja hizo Mbunge Mchafu aliwaahidi wananchi hao na viongozi changamoto hizo amezichukua na kwamba atahakikisha anazifanyia kazi na kuzifikisha katika mamlaka zinazo husika.
Kwa upande wao badhi ya viongozi. CCC katika halmashauri ya kibaha vijijini walimpongeza kwa dhati Mbunge huyo kwa kuwachsngia mifuko ya saruji katika kujenga ofisi ya kata ya kibindu na kukisaidia kikundi Cha kufyatua matofali.
Awali Mbunge wa Jimbo la Kibaha vijijini Michael Mwakamo alisema anamshukutu Mchafu kwa kuamua kufanya ziara yake iliyoambatana na neema ya utoaji wa mifuko ya saruji ambayo italeta tija katika kukuza maendeleo.