Home Michezo MBIO ZA “MAZINGIRA MARATHON” KUFANYIKA DAR ES SALAAM SEPTEMBA 25,2021

MBIO ZA “MAZINGIRA MARATHON” KUFANYIKA DAR ES SALAAM SEPTEMBA 25,2021

0

Mkurugenzi Taasisi ya Amoni Mkonga Chief Promotions Amon Mkoga akizungumza na waandishi wa habarikwenye hoteli ya Kebys Mwenge jijini Dar es salaam leo kuhusu mbio za “Mazingira Marathoni”.

Mmoja wa washiriki wa mbio hizo za riadha katika mashindano hayo Chacha Boyi (27) akielezea ushiriki wake katika katika mbio mbalimbali na atashiriki Mazingira Marathon.

Mkurugenzi Taasisi ya Amoni Mkonga Chief Promotions Amon Mkoga kulia pamjana wenzake wakionesha vipeperushi vitakavyotmika katika mbio hizo.

………………………

Taasisi ya Amoni Mkonga Chief Promotions imeandaa mashindano ya riadha yajulikanayo kama “Mazingira Marathoni” ikiwa lengo ni kuiunga mkono serikali ya awamu ya sita katika kuhamasisha jamii kutunza mazingira.

Akizungumza na waandishi wa habari Mkurugenzi mtendaji wa taasisi hiyo Bw.Amon Mkonga alisema kwamba mashindano hayo yanatarajiwa kufanyika septemba 25 mwaka huu katika viwanja vya farasi ilivyoko jijini Dar es salaam.

Amesema kuwa mashindano hayo yatawashirikisha wanariadha kutoka ndani ya Tanzania na nchi za jirani ikiwemo nchi ya Kenya, ambao washiriki zaidi ya elfu tatu wanatarajiwa kuhamasisha upandaji miti ili kutunza uoto wa asili ambao unaonekana kupotea kila siku zinavyozidi kuendelea.

Amesema kwamba mashindano hayo ya riadha yameandaliwa kwa ushirikiano na wahisani mbalimbali ikiwemo kampuni ya Kinglion ,kampuni ya bia ya serengeti, pamoja na kampuni ya Cocola ambapo kwa pamoja wameamua kumuunga mkono rais Samia Suluhu Hassan wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambaye amekua mstari wa mbele kuhamasisha jamii kutunza mazingira.

Ndugu waandishi wa habari sisi kama taasisi tumeamua kutekeleza agizo la rais wetu mama Samia Suluhu Hassan kama mlivyomsikia amekua akitumia hotuba zake kuhamasisha jamij kutunza mazingira, tumeamua kuandaa mashindano haya ili kumuunga mkono katika kuhamasisha jamii kutunza mazingira” alisema Amon.

Nakuongeza kuwa” kuhusu zawadi za washindi bado tunajaribu kuweka mambo sawa tukikutana katika mkutano ujano na nyinyi tutawatangazia watanzania wajue ni zawadi gani tutatoa kwa wanariadha watakaoshiriki, tunaomba jamii iendelee kutuunga mkono.

Kampuni ya Kinglion ameungana na taasisi ya Amon Mkonga Chief Promotions kuunga mkono mbio hizo kwa kuwa  maisha ya watanzania yanategemea  mazingira lakini pia mazoezi yanasaidia kujenga na  kuimarisha afya zao hususani katika kipindi hiki cha mlipuko wa virusi vya Corona.

“Tuameamua kumuunga mkono , ni jambo zuri sana sisi kama kampuni ya Kinglion tunawajibika pia katika kutunza mazingira kwahiyo mbio hizi zitasaidia sana kuendeleza kampeni hizi za kuhamasisha jamii kutunza mazingira” amesema

Mmoja wa washiriki wa mbio hizo za riadha katika mashindano hayo Chacha Boyi (27) alisema kwamba nia yake nikupata ushindi wa nafasi ya kwanza lakini pia kuitangaza Tanzania kimataifa katika mbio za half Marathon zitakazofanyika nchi za Ulaya.