Katibu Mkuu Kiongozi wa serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Zena Said akimsikiliza Mkurugenzi wa Kampuni kubwa ya uwakala wa elimu nje ya nchi ya Global Education Link (GEL) Abdulmalick Mollel alipotembelea banda hilo wakati wa ufunguzi wa maonyesho ya vyuo vikuu. Wanaoonekana nyuma ni wawakilishi wa vyuo 10 kutoka nje ya nchi ambao wamekuja kwa mwaliko wa GEL kuonyesha kozi mbalimbali wanazotoa kwenye maonyesho ya vyuo vikuu yanayoendelea viwanja vya mnazi mmoja.
Mkurugenzi mwenza wa Kampuni kubwa ya uwakala wa elimu nje ya nchi ya Global Education Link (GEL), Zakia Nassor katikati akiwa kwenye picha ya pamoja na wawakilishi wa vyuo 10 vya nje ya nchi ambao ni washirika wa GEL walioalikwa na kampuni hiyo kuja kushiriki kwenye maonyesho ya vyuo vikuu yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu nchini (TCU).
Wawakilishi wa Chuo Kikuu cha PDEU cha nchini India ambacho ni miongoni mwa vyuo vikuu 10 vya nje ya nchi vinavyoshiriki maonyesho ya vyuo vikuuu yanayoendelea viwanja vya mnazi mmoja jijini Dar es Salaam kwa mwaliko wa Kampuni ya uwakala wa elimu nje ya nchi, Global education Link (GEL) wakimsikiliza mmoja wa wanafunzi aliyekuw akitaka maelezo kuhusu chuo chao.
******************************
*Chuo cha CT nchini India kuwafadhili kwa nusu ada
Na Mwandishi Wetu
CHUO Kikuu cha CT kilichoko katika mji wa Punjab nchini India kimetoa ufadhili wa nusu ada kwa wanafunzi 100 watanzania wanaotaka kusomea ufamasia kwenye chuo hicho.
Ofa hiyo ilitangazwa jana na Mkurugenzi wa Idara ya Kimataifa ya chuo hicho, Sourabh Chaudhary.
Alikuwa akizungumza na wanafunzi na watu mbalimbali wanaotembelea maonyesho ya vyuo vikuu yanayoendekea kwenye viwanja vya Mnazimmoja jijini Dar es Salaam.
Chuo hicho na vingine tisa vimekuja nchini kuonyesha kozi wanazotoa kwenye maonyesho hayo kwa mwamvuli wa wakala mkubwa wa elimu nje ya nchi, Global Education Link (GEL).
Alisema wanafunzi wote 100 watakaopenda kusoma fani hiyo kwenye chuo hicho watapata punguzo Maalum(Scholarship) hadi 50% na utaratibu wa safari utakuwa mwezi huu wa nane.
Alisema kwa wanafunzi ambao bado wako kwenye mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa (JKT) wao wataingia chuoni kuanzia mwezi wa Tisa.
Sourabh alisema urafiki kati ya Tanzania na India ni wa miaka mingi na kwamba serikali ya Tanzania imewekeza kwa kiasi kikubwa sana katika sekta ya afya hivyo ni dhahiri inahitaji wataalamu wa kutosha kuhudumia sekta hiyo.
Alisema pia serikali ya Tanzania imejitahidi
kuboresha miundombinu kwa wanafunzi wa sayansi wakiwepo hao wanaotaka kusoma kozi za afya.
“Kwa kutumia urafiki baina ya nchi hizi mbili uongozi wa chuo umekubaliana ni vyema kuchagua kozi ambayo ina umuhimu na uhitaji mkubwa katika soko la ajira kwa kuipunguzia gharama ili Watanzania wengi waweze kuisoma kwa maendeleo ya nchi na taifa kwa ujumla,” alisema
Aliwahakikishia wazazi kwamba kwamba wanafunzi kutoka Tanzania huwa wanafanya vizuri sana kutokana na maandalizi mazuri yao katika elimu ya sekondari na wengi wao hupokea tuzo mbalimbali kutokana na umahiri wao wa kufanya vizuri,kujishirikisha na michezo na kuonesha tabia njema wawapo chuoni.
Alisema mbali na kozi hiyo ya famasia zipo kozi nyingi akitaja baadhi kuwa ni uhandisi, sanaaa na paramedics na artificial intelligence kwa uchache.