Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Dkt.Faustine Ndugulile akizungumza wakati wa uzinduzi wa studio za redio jamii ya Shirika la Utangazaji nchini (TBC) mradi uliofadhiliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) hafla iliyofanyika leo Julai 26,2021 jijini Dodoma.
MKUU wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka,akizungumza wakati wa uzinduzi wa studio za redio jamii ya Shirika la Utangazaji nchini (TBC) mradi uliofadhiliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) hafla iliyofanyika leo Julai 26,2021 jijini Dodoma.
Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul,akizungumza wakati wa uzinduzi wa studio za redio jamii ya Shirika la Utangazaji nchini (TBC) mradi uliofadhiliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) hafla iliyofanyika leo Julai 26,2021 jijini Dodoma.
Mtendaji Mkuu wa UCSAF Justina Mashiba,akizungumza wakati wa uzinduzi wa studio za redio jamii ya Shirika la Utangazaji nchini (TBC) mradi uliofadhiliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) hafla iliyofanyika leo Julai 26,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt Ayoub Ryoba,akizungumza wakati wa uzinduzi wa studio za redio jamii ya Shirika la Utangazaji nchini (TBC) mradi uliofadhiliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) hafla iliyofanyika leo Julai 26,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt. Faustine Ndugulile, Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Pauline Gekul na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii Mhe. Staslaus Nyongo wakiwa ndani ya Studio za Redio mpya ya Jamii ya TBC leo Julai 26,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt Ayoub Ryoba na Mtendaji Mkuu wa UCSAF Justina Mashiba wakionesha hati ya makabidhiano ya radio jamii ya Tbc ambapo mfadhili mkuu ni mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) Makabidhiano hayo yamefanyika leo Julai 26,2021 Jijini Dodoma.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Dkt.Faustine Ndugulile akikata utepe kuashiria uzinduzi wa studio za radio jamii ya Shirika la Utangazaji nchini (TBC) Kushoto kwake ni Naibu Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Gekul hafla iliyofanyika leo Julai 26,2021 jijini Dodoma.
Mawaziri,Wenyeviti wa Bodi,Wenyeviti wa kamati za Bunge na Wakuu wa taasisi wakipata maelezo ndani ya studio mpya za Radio Jamii ya Shirika la Utangazaji nchini (TBC) leo Julai 26,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt Ayoub Ryoba na Mtendaji Mkuu wa UCSAF Justina Mashiba wakimkabidhi zawadi Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Dkt.Faustine Ndugulile mara baada ya kuzindua studio za redio jamii ya Shirika la Utangazaji nchini (TBC) Mradi uliofadhiliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) hafla iliyofanyika leo Julai 26,2021 jijini Dodoma.
Mkurugenzi Mkuu wa TBC Dkt Ayoub Ryoba na Mtendaji Mkuu wa UCSAF Justina Mashiba wakimkabidhi zawadi Mkuu wa Mkoa wa Dodoma,Anthony Mtaka mara baada ya kumalizika kwa tukio la uzinduzi wa studio za redio jamii ya Shirika la Utangazaji nchini (TBC) Mradi uliofadhiliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) hafla iliyofanyika leo Julai 26,2021 jijini Dodoma.
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari Mhe.Dkt.Faustine Ndugulile akiwa katika picha za pamoja mara baada ya kuzindua studio za redio jamii ya Shirika la Utangazaji nchini (TBC) mradi uliofadhiliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa wote (UCSAF) hafla iliyofanyika leo Julai 26,2021 jijini Dodoma.
……………………………………………………..
Na.Alex Sonna,Dodoma
Waziri wa Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Dkt.Faustine Ndugulile,amezindua studio za TBC redio Jamii Kanda ya Kati ambazo zimefadhiliwa na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote(UCSAF) kwa kushirikiana na Shirika la Utangazaji TBC.
Akizungumza leo Julai 26,2021 jijini Dodoma mara baada ya uzinduzi huo Waziri Ndugulile,amesema kuwa lengo la kuzindua studio hizo ni kuboresha usikivu wa Radio Kanda ya Kati.
” Niwapongeze UCSAF na TBC kwa ushirikiano wenu huu wa kuanzisha Redio Jamii ambayo Sasa inakwenda kuwa na manufaa kwa wananchi wa Mikoa ya Kanda ya Kati, niwahakikishie kama Wizara tutaendelea kushirikiana nanyi katika kuleta usikivu wa mawasiliano,” Amesema Dk Ndugulile.
Aidha Dkt.Ndugulile amesema kuwa Serikali imetangaza zabuni ya leseni na masafa na kuwa tayari imetenga sh.bilioni 2 kwa ajili ya kuboresha usikivu.
“Tayari tumeshatangaza zabuni ya leseni na masafa katika maeneo ambayo hayana usikivu wa redio, tunawaombea Wananchi wenye nia ya kuwekeza watumie fursa hiyo,”amesema
Dk Ndugulile amesema serikali pia inakwenda kufanya mapitio ya tozo za Redio kwenye Wilaya na maeneo ya mipakani ambapo itapunguza tozo hizo lengo likiwa ni kuongeza usikivu kwenye wilaya hizo.
Pia Dk. Ndugulile ametoa wito kwa watanzania kufika kwenye Ofisi za Mamlaka ya Mawasiliano TCRA ili kuangalia Wilaya ambazo tenda hizo zimetangazwa ambapo zitaenda sambamba na punguzo la leseni kwenye Redio hizo.
Kwa upande wake Naibu waziri, Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Pauline Gekul, amesema kuanzishwa kwa redio hiyo ni jambo la kihistoria kutokana na uhumimu wake kwa Taifa hasa katika kufikisha huduma za matangazo ya redio kwa wananchi wa makao makuu na mikoa ya jirani.
“Kituo hiki kimefunguliwa leo tunategemea masuala ya kawaida yanayowagusa watanzania yanakwenda kuzungumzwa na burudani mbalimbali zinaenda kutolewa pamoja na vipindi vinavyokwenda kurushwa ni vya utalii, kilimo na ufugaji, michezo, vijana, michezo, muziki na mila na desturi,” amesema Waziri Gekul.
Aidha, ametoa wito kwa vyombo vya habari nchini kuzingatia weledi na kuhakikisha maudhui yanayokwenda kwa wananchi hayapotoshi na ni ya sahihi na kweli.
Awali Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano Kwa Wote (UCSAF),Justina Mashiba amesema gharama halisi ya ukarabati na ununuzi wa vifaa vya Radio Jamii hiyo ni Sh Bilioni 1.71 huku TBC wenyewe wakitoa Sh Milioni 163.
Mashiba amesema uzinduzi wa Radio hiyo ni muendelezo wa Mfuko huo kurahisisha mawasiliano ambapo awali walishafanya hivyo jijini Arusha na leo ni zamu ya Dodoma.
” Tarehe 30 tutazindua kituo kingine cha kurusha matangazo katika eneo la Kisaki ambacho pia tumekifadhili sisi lengo ni kuhakikisha Radio yetu ya Taifa inasikika kila kona.
“Sisi na TBC tumeendelea kushirikiana kutekeleza miradi ya upanuzi wa usikuvu wa Mawasiliano wenye lengo la kupeleka huduma ya habari kwa wananchi kwa njia ya redio” amesema Mashiba.
Mkurugenzi Mkuu wa TBC, Dkt. Ayoub Rioba amesema kuwepo kwa Redio hiyo, kutasaidia katika kurusha habari za kikanda ili kukuza uelewa wa wananchi kuhusiana na masuala ya kijamii katika maeneo yao.
”Redio hii itaongeza uwezo wa kuandaa vipindi vinavyohusu matukio ya kitaifa ikiwemo vikao vya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na kurusha vipindi vya runinga kutokea Dodoma ikiwemo vipindi vya Jambo Tanzania na TBC Aridhio”amesema Dk.Rioba
Hata hivyo Dk.Rioba ameishukuru UCSAF kwa ufadhili huo na kuwataka wananchi wa Dodoma na Mikoa jirani kuitumia Redio hiyo.