Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani ( wa pili kutoka kushoto) akiangalia jinsi Wajasiriamali ambao wamepewa mafunzo na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo(SIDO) wanavyochuja mvinyo kabla ya kuufungasha. Mkuu huyo wa Mkoa aliokuwa na ziara leo ya kukagua shughuli za Wajasiriamali wanaofanyakazi chini ya SIDO
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani ( wa pili kutoka kushoto) akiangalia Batiki iliyotengenezwa na Mjasiriamali Samila Sumar kwa usimamizi wa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo(SIDO) . Mkuu huyo wa Mkoa aliokuwa na ziara leo ya kukagua shughuli za Wajasiriamali wanaofanyakazi chini ya SIDO
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani ( wa pili kutoka kushoto) akiwa ameshika chupa ya mvinyo uliotengenezwa na Wajasiriamali ambao wamepewa mafunzo na Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo(SIDO) Mkuu huyo wa Mkoa aliokuwa na ziara leo ya kukagua shughuli za Wajasiriamali wanaofanyakazi chini ya SIDO
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani ( kulia) akipata maelezo leo kutoka kwa Mfanyakazi wa Kiwanda cha Maziwa cha Neema cha mjini Tabora Zena Watara jinsi wanavyopima maziwa kabla ya kuendelea hatua nyingine.
Mmiliki wa Kiwanda cha Maziwa cha Neema cha mjini Tabora Samila Sumar (kushoto) akitoa maelezo leo kwa Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani ( wa pili kutoka kushoto) jinsi ya uzalishaji wa maziwa Kiwandani humo. Mkuu huyo wa Mkoa aliokuwa na ziara leo ya kukagua shughuli za Wajasiriamali wanaofanyakazi chini ya SIDO
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani ( wa pili kutoka kulia) akiangalia maandalizi ya chupa za kuwekea maziwa wakati alipotembea Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo(SIDO) leo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani ( katikati) akiwa ameshika chupa ya asali iliyofungwa vizuri baada ya Wajasiriamali kupata mafunzo kutoka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo.
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani ( katikati) akiwa ameshika mshumaa uliotengenzwa na Wajasiriamali baada ya kupata mafunzo kutoka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo. Mkuu huyo wa Mkoa aliokuwa na ziara leo ya kukagua shughuli za Wajasiriamali wanaofanyakazi chini ya SIDO
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani ( katikati) akiwa ameshika batiki iliyotengenezwa Wajasiriamali baada ya kupata mafunzo kutoka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo. Mkuu huyo wa Mkoa aliokuwa na ziara leo ya kukagua shughuli za Wajasiriamali wanaofanyakazi chini ya SIDO
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani mchele uliofungashwa vizuri baada ya Wajasiriamali kupata mafunzo kutoka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo. Mkuu huyo wa Mkoa aliokuwa na ziara leo ya kukagua shughuli za Wajasiriamali wanaofanyakazi chini ya SIDO
Picha na Tiganya Vincent
……………………………………………………………….
Na Tiganya Vincent,RS-Tabora
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amewawataka Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo(SIDO) kutengeneza chupa za vyoo kwa ajili ya kufungashia asali.
Alisema hatua itasaidia kulinda ubora wa asali ya Tabora ambayo inatokana na uepo wa mistu ya miomboi.
Balozi Dkt. Batilda amesema hayo leo wakati wa ziara yake ya siku moja katika Ofisi za SIDO Mkoa wa Tabora kwa ajili kukagua shughuli za Wajasiriamali wadogo ambao wanasimamiwa na Shirika hilo.
Aidha Mkuu huyo wa Mkoa wa Tabora ameitaka SIDO kushirikiana na Shirika la Posta kutangaza ndani nanje ya Nchi bidhaa mbalimbali zinazotengenezwa na Wajasirimali Wadogo wanaowasimamia.
Amesema hivi sasa Posta wanaendesha biashara kwa njia ya mtandao na hivyo ni vema wakaangalia uwezekano wa kushirikiana nao ili kuwainua Wajasiriamali wao.
Naye Meneja wa SIDO Mkoa wa Tabora Samwel Neligwa amesema hivi sasa bidhaa nyingi zinazotengenezwa Wajasiriamali wao zinapatikana katika Matndao wao.