TIMU Harold wakiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Benki ya NMB kabla ya kuanza Ligi hiyo TIMU Maximo wakiwa kwenye picha ya pamoja na watumishi wa Benki ya NMB kabla ya kuanza Ligi hiyo LIGI ya Mpira wa Kikapu ya NMB Madaraka Cup imeanza kutimua
vumbi wikiendi hii kwenye viwanja vya Bandari Jijini Tanga huku Timu Harold
wakiibuka na ushindi wa vikapu 78 -66 dhidi ya Maximo. Akizungumza na Waandishi wa Habari Mratibu wa Ligi hiyo
Riziki Mgude alimaarufu “Kocha Bago”alisema lengo la kuanzisha mashindanbo hayo
lilikujka kutokana na mazoezi waliokuwa wanayafanya kila Jumammosi saa kumi
kwenye viwanja hivyo na walianza kuwa wengi wakaona watengeneze timu tatu
ambazo zitakuwa na upinzani ili waweze kuanza kutengeneza ligi hiyo . Alisema baada ya kufanikiwa kuanzisha ligi hiyo waliona
wawafuate wadau mbalimbali ikiwemo Benki ya NMB ambao walihaidi kuwadhamini
Kombe na Medali lengo likiwa ni kukuza mchezo huo ili waweze kuendelea kufanya
vizuri kwenye mashindano makubwa ikiwemo ya Taifa Cup. Alisema kupitia ligi hiyo ambayo inachezwa kila wikiendi
mpaka Septemba mwaka huu watakuwa wamepata wachezaji wazuri ambao wataweza kuwa
tishio kwenye mashindano ya Taifa Cup na hivyo kufanya vizuri . “Lengo la kuanzisha
Mashindano hayo kwanza ni kurudisha mchezo kwa wadau cha pili vijana waamini
kwamba kupitia huko wanaweze kupata nafasi ya kuja kuwasaidia wengine ambao
wapo chini yao”Alisema. Awali akizungumza katika Mashindano hayo,Meneja wa NMB Tawi
la Madaraka Jijini Tanga Elizaberth Chawinga alisema benki hiyo ipo kwenye
nyanja tatu Elimu ,Michezo na Afya . Alisema baada ya wao kufuatwa na Chama cha Mpira wa Kikapu
Mkoa wa Tanga ambao waliwaomba wawadhamini waliwakubalia na baadae na waliona
waiitwe NMB Madaraka Cup. “Sisi tupo kwa ajili ya kuendeleza vipaji michezo ni ajira
na afya na inatengeneza mahusiano na
niwahaidi kwamba Benki ya NMB tutakuwa nanyi bega kwa bega na tunawakabribisha
wengine wajitokeze”Alisema Meneja huyo. Hata hivyo alitoa wito kwa wana michezo wengine iwapo
wanahitaji kushirikiana nao milango ipo wazi na wamewasaidia vijana hawa kwa
sababu wanajituma “Tunaishukuru Serikali na wadau wa mkoa wa Tanga wanawaunga
mkono hivyo kufungua milango kwa wengine wanaohitaji msaada ikiwemo mchezo wa
pete”Alisema Naye kwa upande wake Mchezaji wa timu ya mpira wa kikapu
mkoani Tanga Patrick Semindu alisema uwepo wa mashindano hayo wao kama vijana
unawaepusha na vitu mbalimbali ambavyo vingeweza kuwa hatarishi kwao. Alisema michezo hiyo ina faida kubwa sana kwani kupitia
michezo mtu anaweza kupata udhamini wa masomo ambao unaweza kuwa na tija kubwa
sana kwake na kwa jamii inayomzunguka. “Lakini pia mazoezi ni moja ya tiba na inaweza kuwasaidia
wengi vijana wengi kupitia mchezo huo vijana wengi wanaweza kupata udhamini wa
masomo na hivyo kupata manufaa makubwa”Alisema |