Home Michezo MUKOKO AWAOMBA RADHI YANGA BAADA YA KUTOLEWA KWA KADI NYEKUNDU

MUKOKO AWAOMBA RADHI YANGA BAADA YA KUTOLEWA KWA KADI NYEKUNDU

0
KIUNGO wa Yanga SC, Mukoko Tonombe, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) amewaomba radhi mashabiki wa timu yake pamoja na makocha baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu katika fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
Simba jana walifanikiwa kutetea taji la ASFC  baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya watani wa jadi, Yanga SC Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Yanga ililazimika kucheza pungufu tangu dakika ya 45 kipindi cha kwanza baada ya Mukoko  kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kumchezea rafu Nahodha wa Simba SC, John Raphael Bocco.

Ni taji la pili mfululizo la ASFC kwa Simba SC na taji la tatu la msimu, baada ya kubeba Ngao ya Jamii na ubingwa wa Ligi Kuu ya Tanzania Bara mapema mwezi huu.