KIUNGO wa Yanga SC, Mukoko Tonombe, raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) amewaomba radhi mashabiki wa timu yake pamoja na makocha baada ya kutolewa kwa kadi nyekundu katika fainali ya Kombe la Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), maarufu kama Azam Sports Federation Cup (ASFC).
Simba jana walifanikiwa kutetea taji la ASFC baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya watani wa jadi, Yanga SC Uwanja wa Lake Tanganyika mjini Kigoma.
Yanga ililazimika kucheza pungufu tangu dakika ya 45 kipindi cha kwanza baada ya Mukoko kutolewa kwa kadi nyekundu kufuatia kumchezea rafu Nahodha wa Simba SC, John Raphael Bocco.