Mbunge wa viti maalumu wa Pwani (CCM) Hawa Mchafu wa kushoto akipeana mkono na Mwenyekiti wa UWT halmashauri ya Kibaha Mji Elina Mngonja mara baada ya halfa fupi ya kumkabidhi mifuko 30 ya saruji kwa ajili ya ujenzi wa mradi wa duka litakalokuwa likitumika maalumu kuuzia biddhaa za wanawawake wajarisiamali .
Mbunge wa viti maalumu wa Pwani (CCM) Hawa Mchafu wa kushoto akikkabidhi mifuko 50 ya Saruji Makamu mkuu wa shule ya sekondari Pangani Diksoni Martini kwa ajili ya ujenzi wa jengo la utawala kwa ajili ya walimu ambao walikuwa wanakabiliwa na changamoto ya kutokuwa na ofisi.
Mbunge wa viti maalumu Mkoa wa Pwani (CCM) Hawa Mchafu akizungumza jambo na baadhi ya walimu ya sekondari Pangani wakiwemo wanafunzi na viongozi wa chama wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukabidhi mifuko hiyo 50 ya saruji.(PICHA ZOTE NA VICTOR MASANGU)
………………………………………………………………..
NA VICTOR MASANGU, KIBAHA
MBUNGE wa viti maalumu Mkoa wa Pwani (CCM) Hawa Mchafu amechangia mifuko 50 ameamua kuchangia mifuko 50 ya saruji kwa ajili ya mradi wa ujenzi wa jengo la utawala katika shule ya sekondari Pangani iliyopo Wilayani Kibaha Mkoani Pwani kwa lengo la kuwakomboa walimu na kuwaondolea changamoto ya ukosefu wa ofisi ambayo kwa sasa inawapelekea kuendeshea shughuli zao za kikazi katika madarasa ya wanafunzi.
Mchafu mbali na kutoa msaada huo wa mifuko ya saruji katika shule hiyo akiwa katika ziara yake ya Kikazi Wilayani Kibaha aliweza pia kuchangia mifuko 30 kwa ajili ya ujenzi wa duka la wakinamama wajarisiamali wa UWT ili waweze kupata fursa mbali mbali za kuuzia bidhaa zao ambazo wanazozizalisha na kupata masoko kwa urahisi.
Katika ziara yake hiyo ya kikazi aliambatana na baadhi ya viongozi wa chama cha mapinduzi pamoja na na baadhi ya wajumbe wa kamati ya siasa ya UWT kwa lengo la kuweza kutembelea miradi mbali mbali ya maendeleo ikiwemo na kutoa msada wa mifuko ya saruji mchanga ikiwemo kusikiliza kero mbali mbali wanazokabiliana nazo na kuzitafutia ufumbuzi na kuwapatia mrejesho juu ya kile ambacho wamekizungumza bungeni katika bajeti ya mwaka huu.
“Ndugu zangu nimeamua kufanya ziara yangu hii ya kikazi ambayo nitapita katika maeneo mbali mbali ambapo nimeweza kuchangia mifuko 50 ya saruji katika shule ya sekondari pangani ambayo itasaidia katika ujenzi wa mradi wa jingo la utawala kwani niamabiwa walimu wamekuwa wakitesekaa sana katika kutekeleza majukumu yake hivyo nina imani hivyo nimewashika mkono katika hili lengo ikiwa ni kuborsha sekta ya elimu na pia nimewashika mkono wanawake wa UWT ambao ni wajasriamali kwa kuwachangia mifuko 30 ili kufanya ujenzi wa duka la kuuzia bidhaa zao,”alisema Mchafu
Pia Mchafu aliongeza kuwa serikali ya awamu ya sita ambayo inaongozwa na Rais Mama Samia Suluhu Hassan lengo lake kubwa ni kuhakikisha kwamba inaboresha sekta ya elimu na kutengeneza mazingira ya kujijisomoa kwa wanafunzi pamoja na kufundishia walimu hivyo ndio maana ameona kuna umuhimu wa kusaidia katika suala la elimu.
Kadhalika aliwahimiza walimu hao wa shule ya Pngani kuhakikisha wanafundisha kwa bidii na kuweka mikakati madhubuti ya kujipanga katika kuongeza kasi ya ufaulu kwa wanafunzi ili siku moja shule ya Pnagani iweze kuwa katika ramani ya kufanya vizuri katika mitihani mbali mbali ikiwemo ile mitihani ya ngazi ya Taifa.
“Katika Mkoa wetu wa Pwani kuna shule mbali mbali za serikali kwa hiyo kitu kikubwa hasa katika shule hii ambayo nimekuja leo kwa ajili ya kusapoti sekta ya elimu inabidi walimu na wanafunzi kushirikiana kwa pamoja lengo ikiwa ni kufanya vizuri katika masomo mbali mbali pamoja na ile mitihani ya Taifa na mimi imani yangu mtaweza kufanikiwa kwa kiasi kikubwa katika suala hili,”alisema Mchafu
Katika hatua nyingine mbunge huyo aliahidi kuendelea kutoa ushirikiano wa dhati kwa kushirikiana bega kwa began a viongozi wa chama wa serikali pamoja na wananchi katika kushiriki mambo mbali mbali ya kimaendeleo na kwamba ataweka utaratibu wa kusikiliza kero na changamoto ambazomzinawakabili ili kuzichukua na kwenda kusisemea pindi anapokuwa katika vikao vya bunge.
Naye kaimu Mwalimu Mkuu wa shule ya sekondari Pangani Diksoni Martini alimpongeza Mbunge Mchafu kwa hatua hiyo ya kwenda kufanya ziaara katika eneo lao na kuwapatia mifuko hiyo 50 ya saruji amabayo kwa upannde wao itakuwa ni mkombozi mkubwa wa kumaliza changamoto hiyo ya kutokuwa na jingo la utawala kwani kwa kipindi hiki wamekuwa wakifanya kazi zao katika mazingira amnbayo sio rafiki sana.
“Mimi kama Kaimu Mkuu wa shule hii ya sekondari Pnagani natoa shukrani zangu za kipekee zaidi kwa Mbunge wa viti maalumu hawa Mchafu kwa kuweza kutushika mkono kwa kutuchangia mifuko hii ya saruji kwa kweli shule ambayo ilianzishwa mwaka 2007 kwa sasa wanafunzi wanasoma darasa moja katika mlundikano mkubwa sana na wakati mwingine darsa moja wanasomo wakiwa idadi yao ni 100 kwa hivyo bado tuna upungufu wa madarasa kama sita vile,”alisema Mkuu huyo.
Mwenyekiti wa UWT katika halmashauri ya mji Kibaha Elina Mgonja alieleza kuwa lengo kubwa la wanawake wajasiriamali ni kujikwamua kiuchumi hivyo msaada huo walioupata kutoka kwa Mbunge kwa ajili ya ujenzi wa duka la kuuza bidhaa zao utakuwa ni mkombozi mkubwa kutokana na kupata sehemu rasmi ambayo watakuwa wanaitumia katika kuuzia bidhaa zao mbali mbali ambazowanazizalisha wao wenyewe.
Naye Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji Kibaha Selena Wilsoni aliongeza kuwa uwepo wa kuanzishwa kwa mradi huo kwa wanawake wa UWT kibaha mji ni moja ya hatua kubwa ya kujileteaa maendeleo na kwamba atahakikisha kwmaba analisimamia suala hilo ipasavyo na kuweza kufikia malengo waliyojiwekea katika kuondokana na wimbi la umasikini.