Wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye maonyesho ya vyuo vikuuu wakipata huduma katika mabanda ya wakala mkubwa wa elimu nje ya nchi Global Education Link (GEL) kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye maonyesho ya vyuo vikuuu wakipata huduma katika mabanda ya wakala mkubwa wa elimu nje ya nchi Global Education Link (GEL) kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa shule mbalimbali nchini wapata maelezo katika mabanda ya wakala mkubwa wa elimu nje ya nchi Global Education Link (GEL) kwenye maonyesho ya vyuo vikuu yanayoendelea kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam
Wananchi mbalimbali waliojitokeza kwenye maonyesho ya vyuo vikuuu wakipata huduma katika mabanda ya Global Education Link (GEL) kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
****************************
· Vyashiriki maonyesho ya vyuo vikuu Dar
Na Mwandishi Wetu
VYUO Vikuu 10 kutoka nje ya nchi viko nchini kwaajili ya kuelezea fani wanazofundisha na kutafuta ubia na vyuo vya hapa nchini katika utoaji wa elimu ya fani mbalimbali.
Vyuo hivyo nane kutoka nchini India na viwili kutoka Ukraine vimekuja nchini kwa mwamvuli wa wakala wa vyuo vikuu nje ya nchi Global Education Link (GEL), kwaajili ya kushiriki maonyesho ya vyuo vikuu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo Vikuu (TCU).
Maonyesho hayo ya siku tano yanayoshirikisha vyuo vikuu na taasisi mbalimbali yalianza jana (Jumatatu) jijini Dar es Salaam katika viwanja vya Mnazi Mmoja na yatanatarajiwa kufunguliwa rasmi leo Jumanne.
Mkurugenzi wa GEL, Abdulmalik Mollel alivitaja vyuo hivyo kuwa ni Chandigarh, Lovely Professional University (LPU), CT, Maharish Makandeshwar, Pandeet Deendayal Energy, Sharda, Rayat Bahra vya India na VN Karazan na Sum State vya Ukraine.
Alisema baadhi ya vyuo vimeahidi kufungua matawi hapa nchini baada ya kuona mahitaji makubwa ya kozi wanazofundisha ambazo wanafunzi wa Tanzania wamekuwa wakizifuata kwenye mataifa yao.
Alisema pia baadhi ya vyuo hivyo vya nje vitaingia makubaliano na vyuo vya hapa nchini kuhusu namna ya kufanyakazi pamoja katika utoaji wa elimu ya juu.
Mollel alisema ujio wa vyuo hivyo ni fursa kwa vyuo vya Tanzania kuangalia namna ya kushirikiana kwenye kozi mbalimbali ikiwemo kubadilishana wanafunzi wanaoendelea na masomo ili kupeana uzoefu.
“Mfano mwanafunzi anaweza kusoma miaka miwili India akaja kumalizia hapa Tanzania na wahapa anaweza kusoma mwaka akamalizia kwenye chuo cha nje, haya ni mambo ambayo vyuo vinapaswa kuangalia namna ya kushirikiana,” alisema Mollel.
Alisema hata vyuo vya nje vinaweza kuitumia fursa hiyo kuangalia kozi ambazo mahitaji yake ni makubwa hapa nchini lakini hazipatikani kwa vyuo vya hapa nchini hivyo kuamua kuweka matawi yake hapa na kuchukua wanafunzi kwenda nchini mwao kusomea kozi hizo.
Mollel alisema ni wakati mwafaka kwa vyuo vya ndani kushirikiana na GEL kutangaza kozi walizonazo ili kuwavutia na kuwaleta wanafunzi kutoka mataifa mbalimbali duniani kusoma kwenye vyuo vyao badala ya kutegemea wanafunzi kutoka nchini pekee.