Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo –Tumbi Dkt . Emmanuel Mrema(kulia) akimwonyesha leo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani(wa pili kutoka kushoto) miche ya mihogo ambayo imezalishwa na Watafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo –Tumbi cha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI) kwa ajili ya mbegu bora za kuuza kwa wakulima.
Kaimu Mkurugenzi wa Kituo cha Utafiti wa Kilimo –Tumbi Dkt . Emmanuel Mrema(kushoto) akimwonyesha leo Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani(kulia) miche ya milimao ambayo imezalishwa na Watafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo –Tumbi cha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI) kwa ajili ya kubadilisha kuwa michungwa
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani(kulia) akitoka kukagua leo mmoja ya shamba la miti asili na matunda pori ambayo imepandwa na Watafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo –Tumbi cha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI) .
************************
Na Tiganya Vincent
RS-Tabora
Mkuu wa Mkoa wa Tabora Balozi Dkt. Batilda Buriani amewaagiza Watafiti kutoka Kituo cha Utafiti wa Kilimo –Tumbi cha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI) kuhakikisha wanaendelea na uzalishaji wa miche miti asili ya matunda na dawa kwa ajili ya maslahi mapana ya nchi.
Amesema nchi nyingi matunda pori yana thamani kubwa sana kwa kuwa yatumika kutengenezea vitu mbalimbali ikiwemo mvinyo.
Balozi Dkt. Batilda alitoa agizo hilo leo wakati akipokuwa na ziara ya kikazi katika Kituo cha Utafiti wa Kilimo –Tumbi cha Taasisi ya Utafiti wa Kilimo Tanzania(TARI)
Amesema Watafiti hao wakasaidia katika kuhakikisha kasi ya upandaji wa miti ya dawa za asili na matunda pori inaongezeka katika jamii kwa ajili ya kuhakikisha kuwa haipotei.
Balozi Dkt. Batilda amesema kwenye matunda pori kuna vitu vingi ikiwemo lishe ambayo ni muhimu kwa ajili ya afya za wananchi.
Amesema kwa TARI wamefanya utafiti na kuonyesha matunda pori yanawezekana kupandwa katika maeneo ya Mkoa wa Tabora ni vena elimu hiyo pia ipelekwe kwa wananchi nao pia waweze kushiriki katika upandaji.